• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

VIONGOZI WATEULE NGAZI ZA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI WAMEKULA KIAPO CHA UTII NA UADILIFU MBELE YA HAKIMU SHILA MKOMA.

Posted on: November 27th, 2019

Leo tarehe 27-11-2019 msimamizi mkuu wa uchaguzi wa serikali zavijiji na vitongoji Jimbo la Longido Bi Natang’aduak Zakayo Mollel amelisimamia zoezi nzima la kuwaapisha viongozi mbalimbali vijiji na vitongoji katika ukumbi wa JK Nyerere ulioko hapa Halmashauri ya Longido. Katika zoezi hilo Hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo wilaya  Longido Ndugu Shila Mkoma Dyumu aliwaapisha takribani viongozi 1225 ikiwemo wenyeviti wa vijiji 49,wenyeviti wa vitongoji 176,wajumbe wa kundi mchanganyiko 608 na wajumbe wa viti maalum 392 kutoka katika vijiji na vitongoji mbalimbali wakiwa wanatoka Chama Cha Mapinduzi CCM.

Pia utoaji wa viapo ulishuhudiwa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya Ndugu Ezekiel Mollel, mwakilishi wa mkuu wa wilaya,afisa kupambana na kuzuia Rushwa Takukuru wilaya Ndugu Ally Mikidadi ,mwakilishi wa OCD,viongozi wa dini na wataalam wa idara na vitengo mbalimbali vya Halmashauri.

Bi.Natang’aduaki Mollel alitumia nafasi hii kuwapongeza sana viongozi hao kwa kupata kibali cha kupewa nafasi ya kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka minne na kuwataka waende wakatatue kero mbalimbali za wananchi na kufanya kazi kwa uadilifu na utii bila upendeleo wowote. Pia alitoa shukrani kubwa sana kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa watendaji mbalimbali kabla na wakati wa uchaguzi kwani zoezi la uchaguzi lilienda vizuri hakukua na vitendo vyovyote vya kuonewa, kupendelewa na uvunjivu wa amani.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya Longido Ndugu Ezekiel Mollel pia aliwapongeza viongozi hao wateule kwa kupata dhamana ya kuwaongoza wananchi na kuwataka waende kuwatumikia wananchi na kutatua kero ambazo zinawafanya wananchi kuichukia na kutoipenda CCM ili kukifanya chama kiweze kukubalika na kupata dhamana tena kwenye chaguzi zijazo. Pia aliwataka kuacha kukisema vibaya chama kwani ndicho kilichowaweka madarakani na kuacha vitendo vya rushwa kwenye kuwatumikia wananchi na kutosita kuwaondoa na kuwafukuza viongozi wazembe kwenye chama.

Mwakilishi wa OCD wilaya pia aliwapongeza viongozi wateule kwa kupata nafasi ya kuwatumikia wananchi na kusema kuwa kutokana na katiba yetu mimi sina chama kazi yangu kubwa ni kuhakikisha wananchi wanafuata sheria bila kulazimishwa endapo itaoneka unavunja sheria basi tunakukamata. Pia aliwataka viongozi waende kusimamia ulinzi na usalama kwenye maeneo yao kwa kuanzia kamati ya ulinzi na usalama katika maeneo wanayoyaongoza na kukemea vitendo viovu ikiwemo rushwa, ndoa za utotoni na wahamiaji haramu.

Afisa wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ndugu Ally Mikidadi aliwapongeza viongozi wateule na kuwaambia kuwa leo mmekuja kula kiapo maana yake ni kwamba unaingia mkataba na serikali hivyo basi ukikutwa na kosa lolote lile uko tayari kushtakiwa kulingana na sheria na taratibu za nchi. Pia aliwataka viongozi wakawe mabarozi wazuri wakukemea na kutokomeza rushwa katika maeneo yao ikiwemo kwenye maswala ya ardhi na kwenye kuwatumikia wananchi kwani rushwa inasababisha vifo na upendeleo kwenye jamii.

Mwisho Bi Natang’aduak alimalizia kwa kuwasihi wenyeviti na wajumbe mbalimbali wakafanye kazi kwa ushirikiano na kuwa mstari wa mbele katika kuwatatulia wananchi kero zao na kuwafichua wale wote wanaofanya vitendo viovu ikiwepo kuwaficha Watoto wanaotakiwa kuanza shule, ndoa za utotoni na ukeketaji.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM