• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATOA TSHS. 4,200,000 KAMA KIFUTA MACHOZI/JASHO KWA WANANCHI LONGIDO

Posted on: May 13th, 2019

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Ofisi ya Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori imetoa malipo ya kifuta Machozi/Jasho cha Tsh. 4,200,000 kwa wakazi 13 wa Wilaya ya Longido waliojeruhiwa/kuumizwa na wengine kuuawa kwa kushambuliwa na wanyamapori hatari/wakali wakiwa katika shughuli zao za kila siku za hapa na pale mwaka 2018 katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Longido.

Wakitoa kifuta Machozi/Jasho  leo Mei 13, 2019 wawakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mkoani Arusha kutoka Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Arusha, ndugu Martina Kalunde (Afisa Wanyamapori) na John Msangi (Mhasibu) mbele ya Afisa Wanyamapori Wilaya ya Longido ndugu Lomayani Saiguran Lukumay kwa wakazi 13 waliomba kuwepo na uthibitisho kutoka kwa watendaji wa Vijiji kuwa wahusika waliyofika mbele yao kwa ajili ya malipo ndio wahusika halali wa matukio hayo ya kujeruhiwa/kuuawa na wanyamapori hatari/wakali.

Martina Kalunde (Afisa Wanyamapori kutoka TAWA) amefafanua kuwa wakazi waliopewa kifuta Machozi/Jasho ni wale waliotambuliwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) na kujaziwa fomu ya Kifuta Machozi/jasho na kutumwa kwa Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Dodoma kuomba malipo kwa wahanga. Baada ya fomu hizo kufika Dodoma Wizara ilimwagiza Mkururgenzi Idara ya Wanyamapori kufanya uhakiki wa madai hayo kwa kufika kwenye Wilaya husika. Kwa Wilaya yetu Uhakiki wa Wizara ilifanyika mwezi wa pili 2019 na kubaini wananchi 11 waliojeruhiwa majeraha ya muda na 02 kuuawa na wanyamapori hatari/wakali. Matukio haya yaliwahusisha wanyamapori aina ya Tembo, Nyati, Simba na Fisi.

Afisa huyo aliendelea kwa kutoa ufafanuzi juu ya malipo hayo na kusema kwamba, kwa mujibu wa Kanuni ya Kifuta Machozi/Jasho ya mwaka 2011, mtu akiuawa na mnyamapori hatari atalipwa kiasi cha shilingi za Kitanzania 1,000,000 kama Kifuta Machozi, 500,000 kama amepata ulemavu wa kudumu na 200,000 kama ni mjeraha ya kupona baada ya muda. Aidha aliorodhesha kwa kuwataja aina wanyamapori waliotajwa kisheria kwa Malipo ya Kifuta Machozi/Jasho na kusema kuwa ni Simba, Nyati, Fisi, Kiboko, Faru, Tembo na Mamba.

Kwa upande wake Afisa Wanyamapori Wilaya ya Longido Lomayani Saiguran Lukumay amebainisha kuwa  kifuta Machozi/Jasho hiki kwa wahanga wa wanyamapori Hatari/wakali ni ishara tosha kuwa serikali iko pamoja na wananchi wake kwa kujali haki na thamani yao.  Aidha aliishukuru serikali kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji (W)  kwa malipo hayo kwa wananchi waliojeruhiwa/kuuawa na wanyamapori huku akisema kwamba malipo hayo yatasaidia kuendeleza uvumilivu wa wananchi kuishi na wanyamapori katika maeneo yao kwa amani.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM