• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

ZIARA YA MBUNGE WA WAFANYA KAZI WILAYANI LONGIDO .

Posted on: November 24th, 2023


"HODI LONGIDO NIMEKUJA  KUWAONA, NIMEFURAHI KUWAONA" Ni maneno yake Mheshimiwa, Daktari Alice Kaijage, Mbunge wa wafanya kazi alipofanya ziara yake na kukutana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido katika ukumbi wa J. K. Nyerere leo tarehe 24 /11 /2023. Akizungumza na watumishi Daktari Kaijage amewaasa wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kutoa huduma stahiki kwa wananchi na jamii inayo wazunguka,sambamba na hilo Mheshimiwa ameiomba idara ya Utawala na Rasilimali Watu kufanya vikao vya mara kwa mara ili kujua changamoto mbali mbali zinazowakuta watumishi kwenye maeneo yao ya kazi sambamba na stahiki zao kama kupanda kwa madaraja, upandishwaji wa vyeo,kuumia kazini na mambo mengi yanayofanana na hayo. 

Mheshimiwa Mbunge ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Daktari Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatazama watumishi wa idara tofauti tofauti kwa jicho la upekee kwani katika miaka mitatu ya nafasi yake kama Rais watumishi zaidi ya 450,000 wamepanda madaraja, wengine wamelipwa stahiki zao za malimbikizo ya mishahara,posho za madaraka  pia imetoa ajira kwa watumishi wakada mbalimbali za utumishi wa umma.

Nae Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Dominic Ruhamvya ameishukuru serikali ya awamu ya sita ndani ya miaka mitatu kwa kuwakumbuka watumishi wa umma kwa kuwapatia stahiki zao pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Clemence Kenyatta amemshukuru Mheshimiwa Alice kwa kuja kuzungumza na watumishi wa umma wa wilayani hapo, pia amemuomba Mheshimiwa Mbunge kufikisha baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo zikiwemo  zile zinazohusiana na stahiki za watumishi, kutoa mafunzo kazini kwa Watumishi wa Serikali ili kuongezea ujuzi wawapo makazini, pamoja na kurudisha sera ya kuwaendeleza watumishi waliopo kazini.

"Asante sana Mheshimwa Kaijage kwa kuja kuzungumzia na sisi watumishi tuliopo Wilayani hapa tunaahidi kutekeleza yale yote uliyo tuagiza kama mlezi na msemaji wa watumishi bungeni tunaahidi kufanya kazi kwa bidii na kuwasaidia watumishi kupata haki na stahiki zao kwa mujibu wa sheria wanapokuwa kazini na hata wakati wanapostaafu"Alihitimiasha Ndugu Peter Matemba Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wilaya.

Ziara ya Mheshimiwa Mbunge Kaijage ni ya siku moja Wilayani humo ikiwa na lengo la kufika na kuzungumza na watumishi na wafanya kazi kwenye Halmasahauri zote  Nchini. 


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi iendelee.





Imeandikwa na Happiness E. Nselu 

Kaimu Afisa Mawasiliano Serikalini Wilaya. 

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO September 04, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • VIONGOZI WA DINI WILAYA YA LONGIDO WATOA TAMKO JUU YA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

    October 23, 2025
  • WANAFUNZI 5,188 KUFANYA UPIMAJI WA KITAIFA DARASA LA NNE LONGIDO

    October 21, 2025
  • WWF YADHAMIRIA KUREJESHA MAZINGIRA ASILIA YA LONGIDO

    October 20, 2025
  • MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA PILI YA MAFUNZO YA WWF KWA VIONGOZI WA DINI, VIJIJI NA VIONGOZI WA KIMILA KUHUSU UHIFADHI WA MAZINGIRA LONGIDO

    October 16, 2025
  • View All

Video

KAMATI YA AMANI NA HAKI WILAYANI LONGIDO YATOA TAMKO LA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.