• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ZIARA YA MHE.DKT.CHARLES MSONDE WILAYANI LONGIDO

Posted on: May 15th, 2024

Naibu katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tamisemi Mh.Daktari Charles Msonde amefanya ziara yake Wilayani Longido Tarehe 14/05/2024 akitokea nchini Kenya alipohudhulia  Mashindano ya riadha ya watoto wenye Umri wa Miaka 12 hadi 15 ambapo watoto walioshiriki Mashindano hayo kutoka Tanzania wameibuka kidedea kwa kushika nafasi ya Tatu kati ya nchi ishirini na moja zilizoshiriki Mashindano hayo huko Nairobi Nchini Kenya.

Mheshimiwa Dkt Msonde alipata wasaa mzuri wa kuzungumza na Watumishi wa Kada ya Elimu Msingi na Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.

Dkt Msonde amewataka wasonge mbele na kufanya Kazi kwa bidii huku Serikali ikiendelea kutatua kero na changamoto zao zinazofifisha utendaji kazi wao.

Changamoto hizo Dkt Cherles Msonde  amezigawa katika sehemu sita zikiwemo Kucheleweshwa kwa upandaji wa madaraja,Ucheleweshwaji wa kubadilishiwa Muundo, Malimbikizo ya Mshahara, Kutopatiwa kwa wakati fedha za nauli na fedha za uhamisho (posho ya kujikimu), sambamba na majibu yasiyoridhisha kwa baadhi ya viongozi wanapotaka kupatiwa huduma au kuomba kupatiwa ufumbuzi wa kero zinazowakibili.

Mbali na uwepo wa Changamoto hizo Dkt Msonde amewaambia walimu kuwa; tayari Serikali kwa kushirikiana na Wizara husika wameshazibainisha kero hizo na Kero nyingi kwa kiasi kikubwa zimeshatatuliwa na zilizo salia zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi. Na amewaahidi walimu waliofika kwenye kikao /Mkutano huo kuwa ni Lengo na Mkakati wa Serikali mara tu ifikapo Tarehe 01/07/2024 kero zote za watumishi hao zitakuwa zimetatuliwa na madeni yao yote yatakuwa yameisha.

Aidha Dkt.Msonde amewaagiza Maafisa Elimu Msingi na Sekondari kuwa karibu na walimu ili waweze kubaini kwa haraka changamoto na kero zinazowakabili kwa lile linaweza kutatulika wajitahidi wanashughulikia kwa haraka sana ili walimu hao waweze kufanya kazi kwa weredi na utulivu.

"Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan anawapenda sana walimu na anajitahidi sana kutatua kero zinazowakabili walimu na anataka tuchape kazi bila kudharauliana na kama tu mashahidi wengi wetu hapa madaraja yamepanda, miundo imebadilika na Madeni ya walimu walio wengi yamelipwa na kwa wachache ambao bado tumeagiza Maafisa utumishi waliopo kwenye Halmashauri zenu na waliopo Ofisi kuu yaani Tamisemi kuchambua upya madai ya mwalimu mmoja mmoja ili waweze kupata stahiki zao". Alisema Dkt. Msonde.

Nae mwalimu Pantaleo Paleso amemshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Tamisemi anaeshughulikia maswala ya Elimu kwa kupata wasaha mzuri wa kuzungumza na walimu pamoja na kuwatia moyo. Sisi kama walimu tunaahidi Serikali yetu kwamba tunakubali kufanya mabadiliko katika Elimu yetu ya Tanzania na tunahakika matokeo yetu ya mitihani yetu yote kuanzia darasa la Nne mpaka ya kidato cha sita yatakuwa na ufaulu wa juu, ili kuweza kupata Taifa Imara na la wasomi.

Akizungumza kwa Niaba ya watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw. Nassoro Shemzigwa amemuahidi Naibu katibu mkuu kuwa watashirikiana bega kwa bega na watumishi sambamba na kujitahidi kutatua changamoto zao makazini.

LONGIDO TUNATEKELEZA KWA VITENDO#

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM