• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WILAYANI LONGIDO

Posted on: March 6th, 2023

Mheshimiwa dkt Festo John Dugange Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Leo tarehe 6/03/2023 amefanya ziara katika miradi mbali mbali ikiwemo shule ya Sekondari Mundarara, kituo cha Afya cha Ketumbeine, Oworendeke, na kuhitimisha kwenye hospital ya Wilaya ya Longido ambako bado ujenzi wake unaendelea kwa baadhi ya majengo machache ili kukamilisha ujenzi huo.

Mheshimiwa Naibu waziri ameiagiza kamati ya wilaya pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama wahakikishe  wanakamalisha miradi yote kwa haraka ili iweze kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.

Mheshimiwa naibu waziri pamoja na kutoa maelekezo kwa viongozi wa wilaya pia amesisitiza matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na Serikali hususani pesa za miradi zinatumika kwenye miradi iliyokusudiwa na serikali na si vinginevyo  na kukamilika  kwa muda uliopangwa.

Naye mkuu wa wilaya ya Longido ndugu Marko Henry Ng'umbi kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Longido ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wake Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuona ipo haja ya  kutoa fedha nyingi  kwenye miradi ya Afya pamoja na shule ili iweze kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Longido ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata changamoto za huduma hizo muhimu.

"Kwa kipindi kirefu wananchi wa wilaya ya Longido  imewalazimu kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo muhimu. Uwepo wa hospital hizi zitawasaidia sana wananchi wote wa Wilaya yangu hasa kina mama ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu mahala pazuri na salama pakujifungulia sasa serikali imewesogezea huduma ya mama na mtoto kwa karibu hivyo nadhahiri kuwa kina mama wote watapata huduma bora za kujifungua bila tatizo lolote kwa usawa na usalama zaidi"Alisema mkuu wa wilaya.

Sambamba na hilo mheshimiwa mkuu wa wilaya ameahidi kutekeleza na kufuatilia kwa karibu ukamilishwaji wa baadhi ya miradi yote yenye changamoto na kuahidi kukamilisha kwa wakati na muda uliowekwa, pia amemshukuru Naibu waziri Dkt Festo John Dugange . Kwa kuridhia kutembelea miradi iliyopo Wilayani humo kwani itasaidia na kuongeza chachu na hali ya ukamilishwaji wa miradi kama ilivyo pangwa.

kwa ziara hii Mheshimiwa naibu waziri wananchi wa wilaya ya Longido na vitongoji vyake inatambua kuwa serikali ipo karibu na wananchi wake hususani wa jamii hii ya wafugaji.

Tunaomba utufikishie salamu zetu za dhati kabisa kwa Rais wetu Mama yetu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza na kuipa kipaumbele wilaya yetu, zaidi sana tunakuomba Mheshimiwa Naibu Waziri usichoke kuja kututembelea mara tu upatapo nafasi"Alihitimisha kwa kusema hayo ndugu Simon Oltosoi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Longido. 

*Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee*

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO September 04, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • VIONGOZI WA DINI WILAYA YA LONGIDO WATOA TAMKO JUU YA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

    October 23, 2025
  • WANAFUNZI 5,188 KUFANYA UPIMAJI WA KITAIFA DARASA LA NNE LONGIDO

    October 21, 2025
  • WWF YADHAMIRIA KUREJESHA MAZINGIRA ASILIA YA LONGIDO

    October 20, 2025
  • MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA PILI YA MAFUNZO YA WWF KWA VIONGOZI WA DINI, VIJIJI NA VIONGOZI WA KIMILA KUHUSU UHIFADHI WA MAZINGIRA LONGIDO

    October 16, 2025
  • View All

Video

KAMATI YA AMANI NA HAKI WILAYANI LONGIDO YATOA TAMKO LA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.