Na happiness Nselu
Mheshimiwa Marco Henry Ng'umbi Mkuu wa Wilaya ya Longido amekemea tabia mbaya inayofanywa na baadhi ya watu hasa katika jamii ya wafugaji waishio Wilaya ya Longido ambao bado wanaendeleza mila mbaya na potofu ya kuwaoza watoto wadogo wenye umri wa kwenda shule,badala yake amewataka kuwa mstari wa mbele kuwasomesha na kuwapatia Elimu iliyo bora ili watoto hao waweze kujitemgenezea msingi mzuri na Imara kwenye maisha yao ya baadae ikizingatiwa Elimu ndio msingi wa Maendeleo ya kila mmoja na jamii kwa ujumla.
Mheshimiwa Ng'umbi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Mnada /Soko la Ketumbeine alipokutana na wakazi wa kata hiyo ya Ketumbeine
Ikumbukwe Serikali inapiga vita sana ndoa za utotoni na sheria iko wazi kwa atakaebainika kufanya ama kutenda matendo hayo ya kikatili kwa watoto.
Jamii imeaswa kuwapeleka watoto wote waliofaulu kwenye shule husika bila kisingizio chochote ikiwemo ada. "Kwa yeyote atakaebainika kumuozesha mtoto mdogo mwenye umri wa kwenda shule nitawakamata na sheria itachukua mkondo wako nataka watoto wote waende shule kwa kuwa madarasa yapo,meza zipo, vitanda vipo, walimu wapo sioni sababu ya kutompeleka mtoto shule" Alisema Mkuu wa Wilaya
Shule zimefungukuwa rasmi tarehe 8/01/2024 wito kwa jamii ni kujitahidi kuwapeleka watoto kwa wakati ili waanze masomo yao kwa utulivu.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM