Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amewataka Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi, Madiwani pamoja na wakuu wa Idara Wilayani longido kuhakikisha wanaondoa Hoja zisizo za muhimu na za kutatulika kipindi cha mikutano ya Robo ili kupunguza idadi ya Hoja katika vikao vya mwisho.
Ameyasema hayo leo julai 11, 2019 wakati akizungumza katika baraza la Madiwani wa kata zote 18 za Longido pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali wa Wilaya hiyo katika mkutano Maalum wa baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Nyerere wilayani hapo.
Mhe. Gambo amesema kuwa Wilaya ya Longido akijaribu kuilinganisha na Wilaya nyingine mbili alizo anza nazo Longido inaonekana kufanya Vizuri zaidi ila tu mapungufu madogo madogo ambayo yanaweza kuzuilika ndio yanayoikabili Longido lakini pia Longido amesema wameweza kuondoa tofauti zao na kufanya kazi kama ndugu jamba ambalo amelipa pongezi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Longido Mhe. Sambore Molloimet amemshukuru Mhe. Gambo kwa kuwa natembelea Wilaya hiyo mara kwa mara huku akimsisitiza kutowakatia tama pale wanapokosea ili kuijenga Tanzania kwa pamoja.
Aidha amewasisitiza kuwa katika vipindi vya robo Wilaya waakikishe kuwasilisha baadhi ya hoja kwa jina la Hoja Maalum ili kuondoa wingi wa hoja hizo.
Naye mkurugenzi mtendaji Mhe. Jumaa Mhina amesema wao kama Halmashauri wajenge utamaduni wa kuwa wanakutana mara kwa mara na wakaguzi huku wakiangalia maara ambapo pana utata na kupatafutia ufumbuzi wa haraka.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM