Halmashauri ya Wilaya ya longido imepokea fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Ujenzi huo utajumuisha majengo yafuatayo ,jengo la wagonjwa wa nje(OPD), maabara,jengo la mama na mtoto,utawala,mionzi,madawa na jengo la ufuaji.
Hospitali hii ikikamilika itahudumia wananchi takribani 142597 wa Wilaya ya Longido ambao walikosa huduma ya hospitali ya Wilaya kwa muda mrefu
Ujenzi umeanza kwa kusafisha eneo la ujenzi wa hospitali hiyo na tutatumia force account kama tulivyotumia kwenye ujenzi wa vituo vya afya na kufanya vizuri,hayo yalisemwa na Eng Dimoso .
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg Jumaa Mhina amesema wanaishukuru sana serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Dkt John pombe Magufuli kwa kutoa fedha hizo za ujenzi wa hospitali ya Wilaya na atahakikisha hospitali hiyo inajengwa kwa kiwango cha juu na kuwa mfano wa hospitali zote Tanzania.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM