Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Ndg. Jumaa Mhina leo tarehe 24/4/2018 amekabidhi miradi ya maji yenye thamani ya Tsh.80,236,460 kwa kamati za maji za kijiji cha Eworendeke na Mtaa wa Namanga juu.
Mradi wa kijiji cha Eworende umegharimu kiasi cha Tsh. 36,065,520/= na mradi wa Mtaa wa Namanga juu umegharimu kiasi cha Tsh. 44,170.940/=.
Mkurugenzi Mhina amekabidhi miradi hiyo kwa kamati za maji zilizopatiwa mafunzo ya jinsi ya kuendesha miradi hiyo.
Kwa upande wao wajumbe wa kamati za maji za vijiji hivyo wamepokea miradi hiyo kwa furaha na kuahidi kuilinda miradi hiyo na kuiendeleza.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM