Leo tarehe 19-11-2020 kampuni ya PowerCorner inayojihusisha na uzalishaji na usambazaji wa umeme utokanao na nishati ya jua katika Kijiji cha Orkejuloongishu kata ya Ketumbeine wilayani Longido imekabidhi msaada wa vifaa tiba katika kituo cha afya Longido ikiwemo vitanda 20 na magodoro 20, mito 40, meza 15, viti 20 na vifaa vya kunawia mikono 71 vyenye thamani ya milioni ishirini na tano laki nane na ishirini na tano (25,825,000/=).
Hafla hiyo iyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Dkt Jumaa Mhina, Mganga mkuu wa wilaya Dkt Justice Munisi na watumishi wa idara ya afya kituoni hapo. Msaaada huo wa vifaa tiba uliozingatia upungufu katika kituoni hapo.
Kampuni ya PowerCorner kwa kuona umuhimu wa kuchangia vifaa tiba ili kuboresha utoaji wa huduma ya afya wilayani Longido imegawa vifaa hivyo pia katika Zahanati ya Ketumbeine ambazo ni vitanda 3 na magodoro 3, mito 6 na meza 3 na vifaa vya kunawia 3 vyenye gharama ya Tsh milioni moja na laki nane hamsini na moja (1,851,000/=). Vifaa hivyo vimetengenezwa na mafundi wazawa kutoka Kijiji cha Orkejuloongishu wakitumia pia vifaa umeme unaozalishwa na PowerCorner.
Mwisho mkurugenzi mtendaji Dkt Jumaa mhina aliwashukuru uongozi mzima wa kampuni ya PowerCorner kwa msaada wa vifaa tiba na kuwaahidi kuwapatia ushirikiano mkubwa wakati wowote na wasichoke kutoa msaada kwani wilaya yetu ni kubwa na vituo ni vingi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM