Mheshimiwa Rahma Kondo Katibu tawala Longido amewataka watendaji wa kata kutoka kata zote kumi na nane za Wilaya ya Longido kuwekea uzito na umakini wa hali ya juu kwenye utendaji kazi wao hasa kuhusu swala zima linalotokana na lishe, Mheshimwa Rahma ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe ya robo ya kwanza cha tarehe 28/11 /2023 katika ukumbi wa J. K Nyerere Wilayani Longido.
Kikao hicho cha tathmini ya Mkataba wa Lishe kimehudhuliwa na wajumbe mbali mbali wakiwemo watendaji wa kata katika kata zote kumi na nane. Mheshimiwa Rahma amewaagiza watendaji kufanya maadhimisho ya siku ya Lishe kwenye kata zao ili kuifanya jamii kuondokana kabisa na tatizo la ukosefu wa lishe kwa wa mama wajawazito na watoto hasa wa chini ya miaka mitano na mara tu wanapofanya maadhimisho hayo kutoa taarifa kwa kamati tendaji zinazoshughulika na uwasilishaji wa taarifa hizo kwenye ngazi husika yaani Mkoani na hatimae kwenye ngazi ya makao makuu OR Tamisemi.
"Ndugu zangu hebu tulichukulie jambo hili kwa umakini mana tulisaini Mkataba hapa mbele ya Mkuu wa Wilaya, si hivyo tu Mkuu wetu wa Wilaya alisaini Mkataba na Mkuu wa Mkoa na kwa utaratibu huo nae Mkuu wa Mkoa aliingia Mkataba kwa ngazi za juu ya uongozi na jambo hili na la Mheshimiwa Rais mwenyewe Mama Samia Suluhu Hassan ambae ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe Taifa"Alisema Bi Rahma Kondo.
Akisoma taarifa ya Tathmini Mkataba wa Lishe Wilaya Ndugu Adelina Kahija taarifa imeonyesha kuwa Halmashauri ya wilaya ya Longido ina jumla ya watoto elfu ishirini na saba na mia nane na kumi na tatu, walio chini ya miaka mitano. Katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2023 jumla ya watoto 13497walifanyiwa tathmini ya hali ya Lishe kwenye vituo vya kutolea huduma ya Afya.
Tathmini ya hali ya Lishe katika Wilaya ilionyesha Kuwa 85.98% ya watoto chini ya miaka mitano wana hali nzuri ya Lishe na 13. 40% wana utapiamlo wa wastani na 0.61%wana utapiamlo mkali.Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imetenga kiasi cha Shilingi 51,084,500 kwa ajili ya utekelezaji wa Afua za lishe. Fedha zilizotengwa kutoka kwenye mfumo wa mapato ya ndani ni shilingi 37,490,000 na mfuko wa Afya ya pamoja shilingi 12,239,000,user fee 630,000 NHIF 500,000, na ICHF shilingi 225,000.
Kwa robo ya Kwanza Julai hadi Septemba 2023 Halmashauri ilipanga kutumia kiasi cha shilingi Milioni 10,904,000 ikiwa ni kwa ajili ya utekelezaji wa Afua za lishe katika wilaya.
Akizungumza kwa niaba ya watendaji wa kata ndugu Kulunjuu N Laizer ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Daktari Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona na kutambua umuhimu wa lishe kwenye jamii hasa hii ya wafugaji waliopo kwenye Wilaya ya Longido na kuahidi kutekeleza yale yote yalio shauriwa na kujadiliwa kwenye kikao hicho cha Tathmini ya Mkataba wa lishe sambamba na kufanya maadhimisho ya Afua za lishe kwa kila kata husika ili wananchi wajue na kuwa na uelewa juu ya hali ya Lishe.
Nae Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Dominic Ruhamvya ameishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele swala hili la lishe kwa jamii, "Ndugu zangu hili jambo la lishe na la muhimu sana na kama tunavyotambua kwa umuhimu wake huo Mwenyekiti wa lishe Taifa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenyewe kwa maana hiyo basi tuweke mkazo sana kwenye kutekeleza shughuli hizi za lishe sambamba na kutoa elimu kwa jamii zetu ili wafahamu umuhimu huo wa lishe bora.
Vikao hivi vya Tathmini ya Mkataba wa lishe ni endelevu ambavyo vinafanyika katika kila robo kwa mwaka.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE.
Imetolewa na Happiness E Nselu
Kaimu Afisa Habari Wilaya.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM