Mheshimiwa Henry Marko Ng'umbi Mkuu wa Wilaya ya Longido amefungua kikao cha kikanuni cha wadau wa Maendeleo NGO'S na CBO leo tarehe 19/06/2023 katika ukumbi wa J. K Nyerere Longido
Kikao hiki kimelenga kuzungumza juu ya matumizi bora ya Ardhi pamoja na uhifadhi wa mazingira hususani katika nyanda za malisho,
Vile vile kikao cha kikanuni kimelenga kujadili shughuli za wadau wa Maendeleo katika kutunza na kuhifadhi mazangira, shughuli hizo ni kama kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira, kusaidi jamii kuwa na uwelewa wa pamoja wakupunguza na kuondoa migogoro inayotokana na ardhi.
Kikao hicho kinaendelea kwa siku mbili katika ukumbi wa J. K Nyerere Longido
Jamhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM