KIKAO CHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA VIASHIRIA VYA MKATABA WA LISHE KATIKA HALMASHAURI WILAYA YA LONGIDO
Mkuu wa wilaya ya Longido mheshimiwa Marco Henry Ng'umbi leo tarehe 31/07/2023 amefungua kikao cha tathmini ya Lishe kilichofanyika katika ukumbi wa J. k. Nyerere Wilayani Longido.
Akisoma taarifa ya Lishe Afisa lishe wilaya ndugu Adelina Kahija, taarifa ya hali ya lishe katika Wilaya ilionesha kuwa 90.51%ya watoto chini ya miaka mitano wana hali nzuri ya lishe na 8.77%wana utapiamlo wa wastani, na 0.72%wana utapiamlo mkali.
Hata hivyo Halmashauri ya wilaya ya Longido ilitenga kiasi cha shilingi 41,187,976 kwa ajili ya utekelezaji wa Afua za lishe kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mheshimiwa Ng'umbi amawataka watendaji wa kata katika Halmashauri kuweka jitihada mahususi za kuhamasisha na kutoa elimu ili kuondoa matatizo na magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora haswa kwa watoto walio chini ya miaka mitano. "Lishe bora kwa mtoto huimarisha Afya na kumpa nguvu mtoto ili aweze kutimiza shughuli zake za kila siku, mtoto mwenye Afya nzuri mara zote anakuwa na furaha hata kwa kumuangalia tu anaonekana anapendeza"Alisema Mheshimwa Ng'umbi.
Kikao cha Tathmini ya Lishe kwa watendaji ni vikao endelevu vinavyofanyika kila robo katika mwaka, ili kujua mwenendo mzima wa lishe kwa watoto katika Halmashauri ikiwa na lengo la kuhakikisha watoto wote wanakuwa na Afya njema.
*Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi iendelee*
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM