Na:Saumu Kweka
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. agDICTO
Kimeta ni ugonjwa unaoathiri Wanyamapori ,binadamu na wanyama wanaofugwa na binadamu,kama vile ng’ombe,mbuzi kondoo nk.Ugonjwa huu ukitokea unaweza kuathiri shughuli za utalii,vifo vya binadamu,wanyamapori na mifugo.
Ugonjwa huo wa Kimeta umeripotiwa kuwepo katika Wilaya za jirani na Wilaya ya Longido ambazo ni Arusha,Arumeru,Moshi,Siha,Monduli na Wilaya ya Ngorongoro ambapo baadhi ya watu wameonyesha dalili za ugonjwa huo,pia wanyama wa kufugwa na wanyamapori wamekufa.
Hivyo Halmashauri kwa kushirikiana na Wawekezaji wake wamefanya kikao ili kujadili jinsi gani ya kukabiliana na ugonjwa huu wa Kimeta unaoripotiwa kuzikumba Wilaya za jirani ,zinazopakana na Wilaya ya Longido,ambayo hutegemea zaidi shughuli za ufugaji wa wanyama.
Timu ya Watalaamu mbalimbali kutoka Halmashauri kutoka idara za Afya,Mifugo,Maendeleo ya jamii,Wanyamapori na Mazingira wataanza kazi rasmi jumanne ya wiki ijayo kuanza kutoa elimu kwa jamii kwa kuzunguka vijiji vyote 49 vya Wilaya ya Longido.
Ili kuhakikisha kwamba jamii inaepukana pamoja na kudhibiti ugonjwa huu hatari wa Kimeta inabidi elimu ya kutosha itolewe kwa wanajamii ,Chanjo kwa mifugo inayofugwa na Wanyama kutengwa yaani wanyama wanaofugwa kutengwa na au kuwa mbali na wanyamapori.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM