Na Johnson Ismail
Maambukizi ya Ukimwi W/longido, yamepungua kwa asilimia kubwa kufikia hadi asilimia1.9% ya aidadi ya walio jitokeza kupima kwenye mkesha wa Mbio za Mwenge uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi Namanga lakini Uzito umeongezeka hadi asilimia 29% ya idadi ya walio jitokeza kupima.
Mkesha huo uli hamasisha Wananchi wengi kupima Afya zao Jumla ya walio jitokeza kupima (VVU)Virusi vya Ukimwi ilikua ni 225,Wanaume159 na Wanawake66, Kati ya hao walio gundulika kuwa na VVU ni 2 MwanaUme1 na Mwana Mke1.
Hata hivyo Walio gundulika kuwa na VVU walipewa Ushauri na Saha na kuunganishwa na huduma za Tiba na Mafunzo hapohapo, Pia ambao hawakuonekana na Maambukizi walipewa Ushauri na Saha ya matumizi ya condom na jinsi ya kuepuka maambukizi ya VVU kwa ujumla.
Pia idadi ya waliopima hali ya lishe na magonjwa sugu yasiyo ambukiza ilikua ni 112, Wanaume 91,Wanawake21 Kati ya hao walio pima Uzito nagundulika kuwa na Unene ulio zidi ni 22 ,Wanaume ni 16,na Wanawake6 Wote walipewa Ushauri wa Lishe Bora na umuhimu wa matunda na mboga mboga mwilini.
Nao walio pima Kisukari walikua jumla yao ni 2, Wanaume ni 16 na Wanawake5.Kati ya hao Mwana ume Mmoja aligundulika kuwa na Ugonjwa wa Kisukari, Na ameshauriwa aendelee kufwatilia Afya yake kila Mara.
Kufuatia ongezeko hilo la Unene wananchi wameombwa kuzingatia Mazoezi ili kuweka miili yao nyema.Pia kwawale wasio na maambukizi yaVVU wasiwatenge waathirika bali wawape ushirikiano wakutosha na Walio gundulika kuwa na VVU wasikate tamaa na kuona huo ndio mwisho wao bali waone huo ndio mwanzo wa maisha
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM