LONGIDO KUPEWA ELIMU YA UJASIRIAMALI.
Longido yapata siku tatu za kujifunza elimu ya ujairiamali, kupitia wataalamu wa shirika la Intergrity Foundation Society lililopo chini ya mkurugenzi Isaac Mnyangi, wameanza kufundisha katika kijiji cha Longido katika ofisi ya kijiji kuanzia tarehe 12.08.2019 hadi 14.08.2019, wamefundisha vitu mbali mbali kama vile kutengeneza batiki, sabuni,na mafuta mgando ya kujipaka. Hivyo wajasiriamali wamefaidi mafunzo hayo na pia kupata vyeti, Isaac amewaasa wajasiriamali hao kuweza kujiajiri ili kuondokana na umasikini na utegemezi. Amehimiza kuwa vyanzo vya vya umasikini nchini ni kutokana na watu wengi kutokujishugulisha katika kazi mbalimbali pamoja na kutomia fursa wanazo pata. Alieleza kwa mfano katika semina hiyo iliyo hudhuriwa na wanawake wengi kuliko vijana, hivyo amewahimiza kuwa elimu ya ujasiriamali ndio mkombozi wa watanzania. Afisa maendeleo wa jamii katika halimashauuri ya wilaya Longido Bi. Grace amewaasa wanawake na vijana kuwa na vikundi vilivyo sajiliwa na vinavyo tmbulika katika halimashauri pia wawe na shughuli maalumu ya kufanya, ndipo watakapo weza kupatamikopo ya serikali alieeleza kuwa aliona uhitaji wa jamii ya longido juu ya ujasiriamali ndipo alipo mualika Isaac kuweza kuja kutoa elimu hii ya ujasiriamali. Aliwaambia wana Longido kuwa kama elimu hii imeonekana kuwa na manufaa kwenu basi tutapeleka hata vijiji vingine ndani ya wilaya yetu ya Longido,ili wana Longido kuweza kujipatia fursa mbalimbali za kimaendeeleo kupitia masomo hayo.semina hiyo imehudhuriwa na watu 200 kwa makadirio ya siku zote za semina, ndani ya kata ya Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM