Taasisi ya chakula na lishe Tanzania ( TCLT), imeendesha semina ya lishe iliyo fanyika tarehe 13 na 14,agosti 2019, katika ukumbi wa OCD Longido,iliyo hudhuriwa na wadau wa afya na lishe wilaya, ikiongozwa na afisa lishe wilaya,wawezeshaji wakiwa ni, Bi.Maria Ngilisho afisa lishe mtafiti mwandamizi taasisi ya chakula na lishe Tanzania (TCLT) pamoja na Prosper Mushi afisa lishe mkoa, wataalamu hawa wamezungumzia zaidi jinsi gani lishe ilivyo bora kwa maisha ya kila mtu. Ameeleza kuwa lishe ni mchakato wa chakula mwilini. Pia katika majadiliano ya wataalamu hao wamesema kuwa ili kuwa na afya bora ni vyema kuzingatia makundi tano ya chakula zinazo weza kumsaidia mwanadamu kuwa na afya bora. Makundi hayo ni; vyakula vya asili yaani nafaka, asili ya wanyama, matunda, mbogamboga na mafuta kama vile karanga,korosho, muwezeshaji wa mada Bi.Ngilisho amesema kuwa katika mazingira yoyote kuna uwezekano wa watu kupata lishe bora kwani ukipika chakula kimoja huchukua karibu aina zote za makundi, hivyo ni vyema jamii kutambua namna ya kupata lishe bora ili kuepukana na madhara mbalimbali kama vile utapiamlo, ameeleza jinsi gani sekta ya lishe inavyo weza kuwiana na sekta zingine kama vile kilimo, mipango, maendeleo ya jamii, elimu, maji na mazingira n.k. pia Bi. Ngilisho ameeleza kuwa ukosefu wa elimu bora pamoja na kukumbatia mila na desturi zilizopitwa na wakati katika jamii huweza kupelekea ukosefu wa lishe bora. Katika kutoa mfano halisi mmoja wa jumbe alieleza jinsi gani jamii za kifugaji (maasai) walivyo na desturi na mila potofu juu ya lishe kwa wanawake wajawazito, amesema kuwa kutokana na ukeketaji wanaofanyiwa wanawake hunyimwa kula vyakula bora, jambo hili hupelekea mtoto kukosa afya toka akiwa tumboni na hata akizaliwa ( siku elfu moja) hivyo hupelekea utapiamlo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM