Wakati Mataifa mbalimbali yanaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani yanayofikia kilele chake hapo Juni 5, 2017, takriban hekta 372,000 za misitu hupotea kila mwaka nchini Tanzania kutokana na shughuli mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Longido nao wanaendelea kuazimisha kwa njia ya kuweka mabango ili kufikisha elimu kwenye jamii kwa njia ya haraka zaidi. Harakati za kufanikisha maanzimisho haya zinafanyaka kadri siku zinavyosonga na kadri ya mahitaji ya kila sku.
Naye Mwandishi Beatrice Lyimo wa Idara ya Habari - MAELEZO anaelezea zaidi kutoka Dar Es Salaam. Kwa miaka mingi siku ya Mazingira duniani imekuwa ikiadhimishwa kwa Wadau katika nchi mbalimbali kuchukua hatua chanya zinazohusu mazingira. Siku hii pia imekuwa ni sehemu ya kampeni ya utoaji elimu juu ya maswala yanayojitokeza kuhusiana na mazingira. Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu inasema “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira” ikihamasisha jamii kuwa na urafiki endelevu na mazingira asilia ambapo kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa mazingira asilia na kuhamasishana ili kuyatunza na kuyahifadhi. Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi Barani Afrika na duniani kwa ujumla imeendelea kuathirika kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo, ufugaji, ujenzi n.k.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM