MABORESHO YA SEKTA YA ELIMU WILAYANI LONGIDO.
Baadhi ya viongozi wa Halimashauri ya wilaya na wanachi eneo la Tinga tinga wakishirikiana kwapamoja katika ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu shule ya sekondari Tinga tinga. Waanchi wameeleza kuwa kwa mda mrefu kumekuwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi na upungufu wa nyumba za walimu. Hivyo kupitia serikali ya awamu ya tano viongozi wameamua kutumia mbinu shirikishi ili kujenga miundo mbinu kwa urahisi kama inavyo onekana wakishirikiana kwapamoja katika kujenga vyumba vya madarasa shule ya sekondari tinga tinga.
Wananchi wa eneo la Tinga tinga wameshukuru kwa dhati kabisa serikali ya awamu ya tano kwa kuboresha maendeleo ya miundo mbinu na elimu katika wilaya yetu ya Longido. Mwenyekiti wa Halimashauri akisaidia kubeba mawe kwaajili ya ujenzi huo.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halimashauri ya Longido Juma Mhina, ameeleza kuwa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita wilaya yetu imekuwa na matokeo mabaya kielimu akitaja shule moja ya misingi ( ilorienito) kushika nafasi ya mwisho kitaifa kutokana na wanachi kutokutoa kipaumbele kwa elimu. Viongozi wa awamu hii tumejitahidi kutokomeza kabisa matokeo mabaya kwa shule zetu. Mwaka huu tumezawadiwa tuzo bora kwa Shule yetu kushika nafasi ya tano kitaifa kwa matokeo ya kidato cha pili.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM