Na Johnson Ismail.
Wananchi wa kijiji cha Nairowa na Namanga Wameonyesha muitikio mkubwa wa Mbio za Mwenge wa uhuru katika vijiji vyao kupita maeneo mengine ya ketumbeine,Gelai Merugoi,Longido,Eorendeke.
Kijiji Cha Nairowa kilionyesha kujitoa kwa kiasi kikwa na kuguswa na uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji kijijini kwao .
Aidha nae mkimbiza Mwenge kitaifa Bw, Amuor Mohamedi Amour aliwaasa wanakijiji wa Nairowa kushikamana na kutunza mazingira kwaajili ya Afya zao, Pia alimtaka Mkuu wa wilaya Mh,Daniel Changula kufanya utaratibu wa kupatikana/kuanzisha viwanda vidogodogo vya Ngozo,Nyama,Maziwa/siagi kwaajili ya kuwanufaisha Wananchi hao wanao jishughulisha na ufugaji.
Pia nao Wananchi wa Namanga Walijitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa shule ya Msingi Namanga kwaajili ya mkesha wa Mwenge wa Uhuru ulio fanyika kijinjini hapo.
Hatahivyo baada ya kuwasili uwanja huo wa mkesha ulio jaa wananchi wa Namanga Ilisomwa Risala kwa Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu Tawala Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa W/Longido na pia mkuu wa wilaya aliwatambulisha Wakimbiza mwenge Kimkoa na kutembelea Mabanda mbalimbali uwanjani hapo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM