MAAFISA UGANI WAELIMISHA JAMII KATIKA MAONYESHO YA KILIMO NA MIFUGO (NANE NANE)
Katika maonyesho ya nane tarehe 08. 08. 2019, Maafisa ugani wameelimisha jamii juu ya kilimo na Mifugo, Afisa Kilimo Emmaanuel Sailevu amesema wametoa elimu juu ya ukulima wa mazao mbali mbali kwa njia ya kisasa kabisa , ambayo ni umwagiliaji, Jamii inatakiwa kujua kuwa njia hii ni muhimu sana kwani mazao hulimwa kwa vipindi vyote vya mwaka bila kujali kipindi cha kiangazi. Kufuatia mradi wa maji kutoka mto simba mazao hayo huweza kulimwa hata eneo la Longido mjini. Maonyesho hayo yamefanyika katika banda la kilimo tingatinga,wataalamu waliweza kuonyesha mazao mbalimbali kama vile; Nafaka( mahindi yanayoweza kukomaa kwa muda wa siku 100 hadi 110), maharage aina mbali mbali za maharage kama ngariase, soya, njegere. Pia kilimo cha mbogamboga kilifundishwa kwa mapana na aina mbalimbali za mboga kama; kabichi, mnafu,spinachi, sukuma wiki, celeri, chainizi, na viungo mbali vya chakula kama vile vitunguu, biringanya, nyanya,karoti.
Pia wataalamu mifugo wameeleza jamii ufugaji wa kisasa na maendeleo ya ufugaji huu wilayani Longido. Katika maonyesho hayo walionyesha aina mbali mbali za mifugo kwa upande wa ng`ombe walionyesha dume la mbegu aina ya sahiwal ambaye ni chotara mwenye sifa kama zifuatazo,huwa na kilo nyingi kuanzia 1000kg na kuendelea,huwa na nyama nyingi, pia ng`ombe jike huwa na maziwa mengi kiasi cha lita 6 (sita) kwa siku, pia wanasifa ya kuwa haraka,na wanaweza kustahimili mazingira magumu,pia wana soko ndani ya nchi na hata nje ya nchi. Pia wataalamu wamifugo walielezea pia aina ya mbuzi waitwao ISIOLO ambapo inasemekana kuwa asili yake ni Kenya lakini aina hii ya mbuzi wametapakaa wilaya nzima sasa kwa asilimia 90%. Pia wana maziwa mengi na yenye ubora wa hali ya juu hutoa kiasi cha lita moja nanusu hadi lita mbili kwa siku, pia wana nyama nyingi na hustahimili mazingira magumu. Katika kuelezea aina ya kondoo wameonyesha aina ya RED MASAI, afisa mifugo amesema kuwa hawa kondoo huwa na tabia ya kupotea sana,hivyo amewaasa wafugaji kuwatunza kwa bidii kwani wanasifa nyingi nzuri na pia hawapatwi na magojwa mara kwa mara na pia asili yao ni Tanzania. Katika maonyesho hayo wataalamu wamewaasa wanajamii wa Longido, kufuga mifugo yenye kuendana na kasi ya kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda ili kuweza kupata malighafi ya kulisha viwanda kama vile ngozi. Pia waliweza kuonyesha aina za malighafi zipatikanazo na mifugo kama vile mikanda ya ngozi, viatu vya ngozi, jamii imehamasihwa utunzaji bora wa mifugo na mazingira, ameeleza afisa mifugo wilaya Nestory Dagharo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM