Leo tarehe 10-10-2019 mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Jumaa Mhina amefanya kikao cha pamoja na watumishi wote wa halmashauri katika ukumbi wa Mwl.Julius Nyerere.
Kwenye kikao hicho kilichoanza saa 9.00 asubuhi katika ukumbi wa halmashauri Mkurugenzi mtendaji aliwakaribisha watumishi wote wapya na wazamani na kuanza kutoa taarifa zote za kiutendaji ikiwemo elimu,michezo,afya na miradi iliyofanyika kabda na baada ya yeye kuteuliwa kuwa mkurugenzi.
Katika sekta ya elimu na mchezo Mkurugenzi alisema kuwa wilaya yetu kwa sasa imepiga hatua kubwa sana. Inafanya vizuri katika mitihani yote ya wilaya na kitaifa pia imetoa mshindi wa kwanza kitaifa katika uandishi wa insha nchi za SADC pia kuweza kuzipandisha shule ambazo zilikuwa zinafanya vibaya kitaifa.katika michezo inayoshirikisha wanafunzi waliopo mashuleni kitaifa inafanya vizuri.
Katika sekta ya afya wilaya imeweza kusimamia ujenzi wa vituo vya afya ikiwemo Eworendeke na Engarenaibor vilivyogharimu takribani bilioni moja na milioni moja kwa pamoja pia kuendelea kusimamia ujenzi wa hospitali ya wilaya wenye gharamaa ya takribani bilioni moja na milioni mia tano.Pia mkurugenzi alisema Kama wilaya tumepata baharia ya kuwa na zahanati ya kisasa iliyoko Olmoti yenye vifaa vya kisasa kabisa ilijengwa na mfadhiri kwa ajili ya kuwasaidia wananchi walikuwa wanasafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma ya afya.
Pia mkurugenzi alitoa tathmini ya miradi mikakati takribani kumi (10) ikiwemo soko la mazao na mifugo,bwawa la kitalii lenye mita 2000,kiwanda cha nyama,mradi wa nyuki,bwawa la samaki, stendi ya kisasa,ambayo ikikamilika itaingiza kiasi cha shilingi bilioni mia moja (100) kwa mwaka.
Kwenye kikao hicho alipata nafasi ya kusikiliza na kutolea ufafanuzi wa maswali na kero mbalimbali wanazozipata watumishi wakiwa katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.
Mwisho kabisa mkurugenzi aliwahasa watumishi wote kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwa kufuata taratibu na sheria zote za kiutumishi bila kuwepo sababu na visingizio vya namna yoyote kwani ikibainika mtumishi amefanya uzembe basi atachukuliwa hatua stahiki za kiutumishi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM