Mkurugenzi mtendaji leo tarehe 26/01/2018 amekabidhiwa majengo yaliyojengwa na mdau Bi Diane Relaigh katika Zahanati Olmot, Diane Relaigh ameweza kujenga Majengo yafuatayo Jengo la upasuaji pamoja na vifaa vyote muhimu vya upasuaji,Wodi za akina mama wajawazito,Wodi ya akina babaPamoja na upanuzi wa zahanati ,Pia Mama Diane ameweza kujenga madarasa sita (6) ya shule ya msingi kwa ajili ya watoto wetu. Makabidhiano yote ya Zahanati na Madarasa yamekabidhiwa leo kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Longido ADV.Jumaa Mhina.Tuna kila sababu ya Kumshukuru huyu Bi Diane Relaigh kwa Alama anayoiacha Olmoti na kwa watanzania .Wadau kama hawa ndio tunaowahitaji ktk kipindi hiki alisema mkurugenzi Mtendaji wakati was makabidhiano hayo.Pia mkugenzi mtendaji amefurahishwa sana kwa ujenzi wa zahanati ya olmotii ambayo ni moja ya zahanati iliyokamilika ikiwa na vifaa vyote muhimu kama mashine xray,kifaa cha kutibu ugonjwa wa manjano pindi mtoto anapozaliwa na manjano madawa ya kutosha pamoja na vifaa vya upasuaji.akizungumza pia katika hafla hiyo mama DIANE amesema anashukuru sana kwa ushirikiano aliopewa na serikali ,mkurugenzi pamoja na wanchi wa olmoti kuweza kufanikisha jambo hili lililogharimu zaidi ya shillingi za kitanzania billion moja.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM