Mwanafunzi Cynthia John Masuka wa kidato cha sita mchepuo wa (CBN) Longido sekondari amekuwa mshindi wa kwanza Tanzania katika uandishi wa Insha. Uandishi huo wa insha ulio jumisha Nchi kumi na sita za (SADC) Chini ya mwenyekiti wa SADC ,Rais wa Jamuhuri ya Muangano wa Tanzania John Pombe Magufuli, uandishi huu uliohusiha shule zote Tanzania kuanzia ngazi ya shule za wilaya, mikoa hadi Taifa kwa ujumla, ambapo walipatikana washindi wa tatu (3) kitaifa, walioweza kushiriki na kushinda uandishi wa Insha( SADC),
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Longido Jumaa Mhina amempongeza mwanafunzi huyo leo hii tarehe 30/8/2019 wakati walipofika ofisini kwake akiambatana na afisa Elimu Sekondari Mwalimu Gerson Mtera,Mwalimu Mkuu Daniel Temu na Mwalimu wake wa somo la kiingereza mwalimu Reachel Boniface. Aliwapongeza wote kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha kuwa wanaitangaza Longido ipasavyo katika sekta ya elimu na kumuahidi mwanafunzi huyo zawadi itakayo tolewa na Halmashauri.
Pia Mkurugenzi alimshauri mwanafunzi Cynthia John Masuka kufanya bidii katika kukuza kipaji chake cha uandishi kwani kitaweza kumsaidia, na baadae anaweza akawa mwandishi bora wa vitabu mbalimbali, pia alimshauri kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa yake ya kielimu.
Mwanafunzi Cynthia J. Masuka aneleza kuwa alifurahi sana kupata ushindi huo, ambapo alizawadiwa tuzo bora ya uandishi wa Insha na Laptop aina ya HP, zawadi hizo amekabidhiwa na Mwenyekiti wa SADC, Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe MagufuliMwanafunzi Cynthia J. Masuke alishukuru sana Walimu wake na wanafunzi wenzake waliompa ushirikiano katika mafanikio yake.
Cynthia J Masuke, alishauri kuwa wanafunzi wenzake wawe na tabia ya kusoma vitabu mara kwa mara kwani itawasaidia kupata misamiati toshelevu katika kujibu mitihani yao pia kushinda nafasi kama alivyo shinda yeye. Alishauri ushirikiano mzuri baina ya wanafunzi na walimu kuwa ni chanzo cha mafanikio bora kwa mwanafunzi, alisisitiza walimu kuwashauri wanafunzi mara kwa mara ili wafanye vizuri katika masomo yao.
Afisa elimu sekondari Halmashauri ya wilaya Longido,Gerson Mtera alimshukuru Mkurugenzi kwa pongezi, pia alimpongeza mkuu wa shule ya sekondari Longido Daniel Temu pamoja na jopo la walimu wenzake kwa jitihada wanazo fanya kuwafundisha wanafunzi na kuipatia shule yetu jina kubwa kitaifa.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM