Mkuu wa wilaya ya Longido Ndugu Frank James Mwaisumbe leo tarehe 17-10-2019 amezindua kampeni shirikishi ya kitaifa kwa ajili ya chanjo ya SURUA RUBELLA (MR) na POLIO YA SINDANO (IPV) katika kituo cha afya cha Longido itakayowahusisha Watoto wote wenye umri wa miezi 9 hadi 59 chini ya miaka mitano. Kampeni hii ni ya siku tano kuanzia tarehe 17-10-2019 hadi 21-10-2019 katika vituo mbalimbali ndani ya wilaya yetu ya Longido kila siku kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.
Katika kampeni hiyo mganga mkuu wa wilaya Dokta Justice Munisi alitoa takwimu ya utoaji chanjo hizi ambapo kitaifa ilianza mwaka 2014 na ilipangwa itakuwa inafanyika kila baada ya miaka minne kwa lengo la kampeni hii ni kuhakikisha Watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano wanapata chanjo hii.
Pia Dokta Justice Munisi alisema kuwa kwa mwaka huu 2019 wilaya ya Longido imepanga kuwachanja Watoto 23691 kwa chanjo ya SURUA RUBELLA na 10890 kwa chanjo ya POLIO YA SINDANO.
Mwisho mkuu wa wilaya ndugu Frank Mwaisumbe aliwasisitiza wananchi juu ya umuhimu wa chanjo kwa Watoto wetu mana bila chanjo hata sisi tusingekuwa hapa na kuwahasa kuwa wajumbe hata kwa wazazi ambao hawakuwaleta Watoto hapa leo wawalete ili wapate chanjo mana itakuwa kazi bure kwani lengo ni kila mtoto apate chanjo hii. Pia alisisitiza kuwa chanjo hizi ni bure zinapatikana bila malipo hii inatokana na ulipaji kodi wetu mzuri ndio mana serikali imeamua kutuletea chanjo bure.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM