Mkuu wa wilaya ya longido Mh. frank J Mwaisumbe amewakabidhi vijana wa wilaya ya Longido pikipiki 12 leo tarehe 13/11/2018.
Akikadhi pikipiki hizo mh mkuu wa wilaya amewahasa vijana hao kutumia bodaboda kwa kuendeleza na kuinua uchumi wao ,
hata hivyo amewahasa kutunza pikipiki hizo ili waweze kurejesha mrejesho kwa wakati ili vijana wengine wafaidike na mrejesho huo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Longido Advocate Jumaa Mhina amesema, hii ni historia katika wilaya ya Longido ikizingigatiwa kwamba siku chache zilizopita halmashauri ilitoa zaidi ya milioni 42 kwa vikundi mbalimbali katika wilaya ya longido na akaahidi tena fedha nyingine kwa ajili ya vijana na walemavu
Pia ameawataka vijana kutumia hizo fursa kujikwamua kiuchumi na kuachana starehe zisizo na maana bali wapige kazi kuiunga mkono serikali inayoongozwa na Mh Rais John Pombe Magufuli kwa kuchapa kazi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM