Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Longido Dkt Jumaa Mhina leo tarehe 14/08/2020 amekutana na vyama vya siasa vitakavyo shiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Vyama vilivyoshiriki kikao hicho ni Chama cha Mapinduzi (CCM) ,Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), Msimamizi wa Uchaguzi akiongea wakati wa kikao hicho, amevitaka vyama vya siasa kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu na kuzingatia muda wa kampeni utakapofika kuwa ni kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni, Lakini pia kuleta ratiba zao za kampeni mapema ili waweze kukubaliana,Pia Dkt Mhina amevitaka vyama hivyo kurudisha fomu tarehe 25/08/2020.
Vilevile Msimamizi wa uchaguzi amevijulisha vyama kuwa kamati za maadili zitaundwa kuanzia ngazi ya jimbo mpaka kata na kuwataja wajumbe wa kamati hizo. Dkt Mhina alivishukuru vyama vyote vilivyoshiriki kikao hicho na kuwakabidhi sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa, Kitabu maelekezo kwa mawakala wa vyama vya siasa na kitabu cha maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 na kuwataka kila chama kutimiza wajibu wake.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM