Kiongozi wa mbio Za mwenge Bwana bwana Amour Mohamed Amour amekimbiza mwenge wa uhuru katika Halmashauri ya wilaya ya Longido. Mwenge wa uhuru umepokelewa katika kijiji cha Gilai Merugoi muda wa mbili asubuhi na kuzindua Mradi wa Madarasa matatu yenye thamani ya zaidi sh 75 Milioni shule ya Natron Flamingo.
Baada ya kuzindua Mradi huo mwenge ulikimbizwa mpaka jujiji cha Mailowa ambapo Mradi Mkubwa wa Maji ulizinduliwa wenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 1.6
Mwenge wa uhuru uliendelea kukimbizwa mpaka mji wa Longido makao makuu ya wilaya nakuzindua Mradi wa jengo la X ray lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
Baadae mwenge ukaelekea eneo la Mradi mkubwa wa MIVARF wa soko la kisasa la mifugo kijiji cha Ewerendeke mradi huo ulizinduliwa ukiwa na thamani ya zaidi ya sh bilioni 1.9
Hata hivyo Mwenge wa uhuru ulikesha katika Mji wa mpakani Namanga ambapo shamra shamra zilipamba moto Usiku kucha.
Katika sheŕehe hizo mambo mengi yamefanywa ikiwa na pamoja na kupima Afya magonjwa yakuambukizwa na yasiyoambukizwa. Hata hivyo katika upimaji wa VVU watu wawili tu walibainika kuwa na VVU sawa na asilimia moja.
Hata hivyo kilele cha Mbio za mwenge kilihitimishwa viwanja vya oldonyo sambu kwa kusomwa taarifa ya mbio za mwenge wilayani Longido na Mkuu wa Wilaya Bwana Daniel Chongolo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM