Taasisi ya Mwalimu Nyerere iliweka kambi wilayani Longido kwa siku mbili kwa lengo la kuhamasisha umuhimu wa watanzania kutunza Amani na umoja ambazo ndio nguzo ya maendeleo kama Mwl Nyerere alivoagiza kipindi cha uhai wake na ikiwa ni kazi kubwa ya tasasisi hiyo kuhubiri Amani na umoja Tanzania na hata duniani kote.Mkurugenzi mtendaji wa Mwl.Nyerere foundation , Mzee Joseph Butiku alieleza kwa undani na mapana zaidi Nafasi ya viongozi wa ngazi ya serikali za mitaa katika kusimamia katiba , na kuawaeleza viongozi hao ambao ni wenyeviti wa vijiji na watendaji wa kata kua wananchi wanapaswa kusimamiwa kwa mujibu wa katiba na sheria zilizowekwa ili kuepuka migogoro na wananchi na pia viongozi hao wasisite kuwaelimisha wanannchi wao kuhusu umuhimu wa amani katika jamii ili kuwa na jamii salama na yenye kufanya kazi kwa juhudi ili iweze kujipatia maendeleo.
Mzee Gallus Abedi msaidizi maalum wa Mkurugenzi wa Tasisi ya Mwalimu Nyerere pia alizungumzia juu ya namna uongozi wa kijiji , kata , wilaya , mila na vikundi mbalimbali wanavyopaswa kusimamia Amani , Umoja na Maendeleo ya wananchi akisema kua viongozi wanapaswa kua mstari wa mbele kuzungumza habari ya Amani kila wanapokutana na wananchi kwani Amani na umoja wa wananchi hao utawapa nafasi ya kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano hivyo watakua na nafasi ya kuendelea, Mzee Abedi pia alisisitiza kua viongozi hao wanapaswa kulinda rasilimali zilizopo na kuzisimamia kikamilifu rasilimali hizo kama ardhi ili kuepusha migogoro itakayochochea upotevu wa amani katika jamii wanazo zisimamia kama viongozi. Mwisho wazee hawa kutoka Taasisi ya mwalimu Nyerere walishauri serikali hasa Halmashauri ya Wilaya ya Longido kushuhulikia mambo yanayowahusu Wananchi wa Wilaya hiyo bila kuchelewa hasa mambo yanayohusu mipaka na umiliki wa ardhi ili kuepusha upotevu wa Amani kwenye jamii ya watu wa Longido. Ikiwa kama dhumuni la taasisi hiyo kuhubiri Amani, umoja na maendeleo ya wananchi , Uongozi wa wilaya ya longido uliwashukuru Taasisi hiyo na kuahidi kufanyia kazi ushauri na maelekezo ya wazee hao wa Taifa la Tanzania na Taasisi ya Mwl .Nyerere.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM