Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesaini kandarasi zenye thamani ya dola lukuki za Marekani mjini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka Mto Simba na kupeleka katika Halmashauri ya Longido. Katika Hafla hiyo walioishiriki ni watu Mbalimbali kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Longido ambao ni Mheshimiwa Molloimet Sabore(Mwenyeki wa Halmashauri) na Wakili Jumaa Mhina (Mkurugenzi Mtendaji)
Mradi huu ni moja ya Ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dr.John Joseph Pombe Magufuli katika kauli mbiu yake ya Hapa kazi Tu na sera yake nzuri ya Tanzania ya Viwanda.
Mungu Ibariki Tanzania Mungu ibariki Longido
Imeandaliwa na Joseph Peter Mkumbwa (ICTO)
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM