NA.Johnson Ismail.
Shule ya Msingi Kitumbeini Imefanya Mahafali ya Kuwaaga Wanafunzi wa darasa la Saba wanao tarajia kufanya Mtihani wao Wiki ijayo tarehe 4 na kuhitimisha tarehe7 mwezi wa 9 Mahafali hayo yaliyo hudhuriwa na Viongozi wa Halmashauri, Dini, Kata, Vijiji, Vitongoji, Walimu ktoka shule mbalimbali za wilaya,Wazazi na Wageni wengine wengi kwaajili ya kuwaaga wanafunzi hao.
Hata hivyo Mgeni Rasmi aliye hudhuria kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Longido Mwl.Gerson Mtera Ambaye ni Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya W/Longido. Alianza Hotuba yake kwa kuwashukuru watu wote walio hudhuria wakiwemo World Vision wasaidizi wa kubwa wa maendeleo ya shule Wanafunzi wanao hitimuwazazi kwa walimu wote.
Aidha Mwl,Mtera Alitoa Wito kwa Wazazi kugharamikia mambo ya Msingi kama Sare,Matibabu,na kuhakikisha wanachangia katika kuboresha Miundo mbinu naAliwasisitiza Wanafunzi na Wazazi kuhusiana na umuhimu wa elimu na Kuachana na Ujinga wa ktosoma,Utoro ama kutosomesha watoto kwasababu ya shughuli za ufugaji, kushurutisha watoto kuto kukufanya vizuri darasani ili kuoana ,pia Swala la mimba ambalo hawata fumbia macho na kuwa taka wanafunzi kuzingatia swala la Elimu tu na si maswala mengine.
Hata hivyo nae Afisa Elimu Taaluma wa Halmashauri alizungumzia Swala la Ufaulu mzuri wa wanafunzi wa Kitumbeini kuanzia Mwaka 2014 hadi Mwaka jana ambapo mwaka jana shule ili weza kuwa ya kwanza Kiwilaya na Kimkoa na kuwaasa kuwa makini katika ujazaji wao wa Mitihani Kwana kushuka kwa Ufaulu kuna letwa na wao wenyewe pia kupanda kwa ufaulu kunachangiwa na wao wenyewe na kuwaambia ilishule ibaki kuwa na Sifa nzuri ni lazima wajitahidi.
Pia Mahafali hayo yali hitimishwa na Harambee iliyo fanyika kwaajili ya kupata fedha za ujenzi wa nyumba ya walimu,Harambee hiyo iliyo simamiwa na Mgeni Rasmi ili kusanya kiasi cha Sh; LakiTanoelfu hamsini na Tano na Miatano keshi, na Ahadi Milioni Sita kutoka kwenye vijiji. Mgeni rasmi mwl Mtera alimalizia Harambee kwa kuomba uaminifu katika Ahadi zilizo ahidiwa ili kuendelea kujenga shule zetu.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM