Wilaya ya Longido katika kuadhimisha kilele cha siku ya Ukimwi Dunia inayofanyika Tarehe 01-12-2019 kila mwaka leo Tarehe 02-12-2019 imefanya sherehe ya kuadhimisha kilele cha siku ya Ukimwi Duniani katika eneo la wazi lililopo katika kata ya Mundarara.sherehe hizo iliyohudhuriwa na mgeni rasmi Ndugu Toba Nguvila akimwakilisha mkuu wa wilaya Mhe Frank Mwaisumbe, pia walihudhuria watumishi wa idara ya afya na maendeleo ya jamii wilaya, mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia, viongozi wa vijiji na vitongoji na viongozi wa dini.
Pia kwenye sherehe hizo zilizohudhuriwa na wananchi wengi wa kata hiyo hasa wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya Rubi ziliambatana na utoaji wa elimu juu ya Ugonjwa wa UKIMWI,upimaji wa afya na burudani kutoka katika vikundi mbalimbali vya dini, vijana na akina mama kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Longido.
Katika sherehe za MAADHIMISHO hayo yaliambatana na upimaji wa afya walijitokeza takribani zaidi ya wananchi mia tatu 300 kupima afya zao kwa hiari.
Mgeni rasmi Ndugu Toba nguvila akiwa kwenye sherehe hizo aliwahasa Sana wananchi wa Mundarara juu ya umuhimu wa kuadhimisha sherehe hizo na kuwapongeza Sana wananchi na viongozi wao kwa kuhudhuria kwenye sherehe hizo. Moja ya faida hizo Ni kutoa elimu kuhusu ugonjwa hatari wa UKIMWI ikiwa pamoja ya jinsi gani mtu anaweza kupata maambukizi,jinsi ya kujikinga na maambukizi na Kama utakutwa na maambukizi Ni jinsi gani unaweza kuishi kwa matumaini.
Kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema kuwa hakuna maambukizi mapya Bali tunajikinga kuzuia ueneaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI ndugu mgeni rasmi aliwataka wananchi kuacha kuendelea Mila potofu ambazo zinachangia ueneaji wa ugonjwa huu ikiwemo ukeketaji na kuoa wake zaidi ya mmoja. Pia aliwataka wananchi kumrudia Mungu wao katika Imani zao Kama wameshindwa kabisa kujizuia kutumia njia hizi potofu.
Nae kiongozi wa Mila Laingwanan alipata Nafasi ya kuielimisha wananchi waliohudhulia katika sherehe hizo na kuwasisitiza wananchi wa jamii ya kimasai kuacha kabisa ukeketaji na ndoa za wake zaidi ya mmoja kwani ndio Mara nyingi zinasababisha ueneaji wa ugonjwa wa UKIMWI.
Afisa maendeleo wilaya Bi Grace mghase aliwata wananch KUJITOKEZA kwa hiari kwenda kupima afya zao kwani kufanya hivyo kutawafanya kuwa na uhakika kabisa wa afya zao na kuwaomba kuacha KUWANYA NYAPAA wale ambao wanakutwa na virusi vya UKIMWI kwani kufanya hivyo kutawafanya wawe huru kwenda kupima afya zao kwa kujua kwamba jamii haitaninyanyapaa hata Kama nitagundulika na virusi vya UKIMWI.
Mwisho dokta Matrona mwakilishi wa mganga mkuu wilaya dokta Justice Munisi nae aliwataka wananchi kuwa na tabia ya kwenda kwenye vituo au zahanati kupima afya na sio kusubiri mpaka kwenye siku ya maadhimisho. Pia aliwashukuru wananchi wote kwa kujitoa kwenye siku hiyo na kuonyesha muitikio mkubwa na kwenda kupima afya.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM