Leo tarehe 02/09/2019 shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu nchini Tanzania wilaya ya Longido (SHIVYAWATA) imeandaa hafla katika kata ya Mundarara iliyohudhuriwa na mgeni rasmi Mkurugenzi mtendaji hamashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Jumaa Mhina,pamoja na viongozi mbalimbali akiwepo Diwani wa kata hiyo ndugu Alais Mushao,watendaji na wenyeviti wa vijiji, Pia hafla hiyo iliyoambatana na harambee ya uchangiaji fedha ilisimamiwa vizuri kabisa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Jumaa Mhina na kufanikisha kukusanya kiasi cha Tshs. Milioni tano (5,000,000/=) kwa ajili ya uboreshaji wa huduma mbalimbali zinazofanya na shirikisho hilo kuwasaidia watu wenye ulemavu wanaoishi katika wilaya yetu ya Longido.
Aidha Mkurugenzi mtendaji hamashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Jumaa Mhina alisimama na kusema pongezi kubwa kabisa ziende kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Raisi wetu Dr John Pombe Magufuli kwa kuamua kutenga asilimia kumi 10% ya vijana,wanawake asilimia mbili 2% iende kwa walemavu, pia amesema mwaka huu wameshatoa kiasi cha Tsh milioni mia na thelasini mbili (132,000,000/=) tayari kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu. Pia mkurugenzi mtendaji aliwataka jamii ya watu wenye ulemavu kutengeneza vikundi kwa ajili ya kuwasaidia kupata mikopo hiyo isiyo na riba asilimia 2% kwani fedha hizo zitawasaidia katika kujikwamua na ugumu wa Maisha.
Pia katika hafla hiyo mwenyekiti ndugu Elisha Maala Millya wa shirikisho la watu wanaoishi na ulemavu wa aina mbalimbali ikiwemo viungo vya mwili, ulemavu wa Ngozi na kuona taklibani elfu tatu na mia tano (3,500) katika wilaya Longido alisoma risala fupi ikielezea changamoto na mafanikio mbalimbali ambayo wameyapata tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo.
Mwenyekiti wa shirikisho hilo ndugu Elisha Maala Millya alibainisha baadhi ya Changamoto wanazozipata watu wenye ulemavu zikiwemo:- kunyanyapaliwa, kutokuwa na ofisi maalumu, kutowapeleka Watoto wenye ulemavu shuleni, swala la ajira, changamoto ya usafiri, ubovu wa miundo mbinu sio Rafiki kwao na mwisho alimalizia na kutokuwepo na bajeti ya kutosha kwa watu wenye ulemavu wilaya ya longido.
Pia mwenyekiti ndugu Elisha Maala Millya alibainisha baadhi ya mafanikio ambayo wameyapata Tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo yakiwemo ;- kupatiwa mikopo ya asilimia mbili 2% na kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali, kupata baiskeli hamsini (50) aina ya wheelchairs kutoka katika kampuni ya Tanzania Big Safari, kupata ofisi eneo la orbomba japo inahitaji ukarabati kidogo pamoja na samani za ofisi, kufanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa wilaya yetu, kukutana na watu wenye ulemavu kutoka katika kata mbalimbali za wilaya ya Longido na kuweza kufanya vikao mara tatu kwa mwaka kama katiba ya a shirikisho inavyosema.
Mwisho mwenyekiti ndugu Elisha Maala Millya alimalizia kwa kutoa shukrani nyingi kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kujali sana watu wenye ulemavu kwa kuteuliwa wizara ya watu wenye ulemavu pia kuwashirikisha katika ngazi mbalimbali zikiwemo uwaziri,ubunge pamoja na ubalozi,pia kututengea asilimia mbili 2% ya pato la serikali kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya watu wenye walemavu. Pia kumshukuru mkurugenzi mtendaji Ndugu Jumaa Mhina kwa kuweza kufika katika hafla hiyo kwa kuacha majukumu mengine ya kiofisi na kuja kuhudhuria hafla hiyo na kufanikisha kupatikana kwa kiasi cha fedha Tsh milioni tano (5,000,000/=).
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM