TASAF YAENDESHA MAFUNZO KWA WAWEZESHAJI KUTOKA KATA MBALIMBALI ZA WILAYA YA LONGIDO.
Akifungua mafunzo hayo kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya longido ndugu Nestory Dagharo amesema wawezeshaji hawa watapata mafunzo haya ya siku 5 yatawasadia kukabiliana na chanaganoto mbalimbali watakayo kutana nayo pindi watakapo kuwepo vijjini wakitoa mafunzo ,
Aidha amesema kuna vikundi 249 ya wanonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini kataka wilaya yetu ya longido na mafanikio ni makubwa sana kwani mpaka sasa wamekwisha wekeza zaidi karibu million 57 ,pili wanaonufaika na TASAF wamepata mafunzo mbalimbali ,wamenufaika na masanduku na mashajala na mihuri kwa ajili ya kuwezesha ukopeshwaji wa fedha kwa wanakikundi
Matumaini yangu ni kwamba mafunzo haya yatasaidia vikundi hivi kwa mafanikio makubwa kwenye vikundi mbalimbali katika halmashauri yetu
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkuu wa idara ya malalamiko kutoka makao makuu ndugu Makunja Dismas Yusuf amesema lengo kuu la mpango huu ni kukuza utamaduni wa kijiwekea akiba kwa kaya maskini ili waweze kukabiliana na dharura na mahitaji ya msingi kwa familia maskini na kujenga uwezo wa kujiamini
Mafunzo hayo yataendeshwa kwa siku tano na imehuduriwa na wawezeshwaji wa maeneo mbalimbali ndani ya halmashauri ya Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM