Na:Saumu Kweka
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. ICTO
Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro ilianzishwa mwaka 1959,hifadhi ya eneo la Ngorongoro iliingizwa kwenye orodha ya maajabu ya urithi wa dunia mwaka 1979 baada ya kuwa na vigezo 3 vya maajabu ya urithi wa dunia.
Sababu zinazopelekea kurejea kwa mpango wa usimamizi ni mahitaji na shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama vile Miundombinu,Uwekezaji,Biashara na huduma za kijamii,ongezeko la mahitaji ya ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali na mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ajili ya maendeleo .
Malengo makuu ya urejeaji utakuwa ni,Kutatua au kudhibiti migogoro ya matumizi bora ya ardhi,kupanga matumizi bora yaardhi kwa uhifadhi endelevu wa hifadfhi ya Ngorongoro na Kuangalia mienendo ya matumizi ya ardhi kutoka miaka 10 iliyopita.
Njia zinazotumika katika kurejea mpango huo ni tathmini shirikishi ya jamii,hii ndiyo itakuwa njia kuu ya urejeaji wa mpango ,ambapo wadau wote wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro watashirikishwa kwa namna moja au nyingine katika hatua zote kuanzia uhamasishaji ,upangaji na hadi utekelezaji.
Aidha matokeo ya uhamasishaji yanayotarajiwa ni,Kupatikana kwa maji safi na salama kwa binadamu,mifugo,na wanyamapori,kuongezeka kwa mapato yatokanayo na utalii,kuboreka kwa maisha ya wenyeji wa hifadhi ya Ngorongoro na kupunguza kwa uharibifu na uchafuzi wa mazingira.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM