MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA YATOA SIKU MBILI WATUMISHI KUWASIJILI LAINI .
Leo hii tarehe 21 na 22. 08.2019 katika halimashauri ya wilaya Longido ndani ya ukumbi wa nyerere inaendelea usajili wa laini za aina zote kufuatia tangazo la TCRA.
Katika kuboresha usajili wa laini za simu, mamlaka ya mawasiliano Tanzania ilizindua zoezi la usajili wa laini za simu mnamo tarehe 01.05.2019 unaohusisha uchukuaji wa alama za vidole (Biometric simcard registration)nchini. Ili kuongeza kasi ya wananchi wengi kusajili laini zao, mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania kwa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano imepanga kuendesha zoezi la usajili kwa watumishi wa halmashauri yako katika tarehe tajwa.zoezi hili litaendeshwa kuanzia saa3: 00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. Inalenga kuwapa watumishi fursa kusajili laini zao mapema kabla ya mda wa ukomo wa zoezi husika mwezi Disemba 2019.
Mwandisi mwandamizi mamlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazini, Kaaya Jan, amesema kuwa usajili huu ni wa muhimu sana kwani inasaidia usalama mtandaoni na kurahisisha kujua wanao iba pesa za watu kwa njia za kimtandao. Anawasa watumishi kusajili mapema ili kuepuka usumbufu wa kufungiwa laini baada ya zoezi hili.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM