Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank James Mwaisumbe amewataka wadau wa sekta ya Afya ya akina mama na watoto mkoa wa Arusha kuhakikisha wanashiriki katika kumaliza vifo vya Uzazi wa akina mama na Watoto.
Ameyasema hayo mapema leo wakati akifungua kikao kazi cha kujadili namna ya Kupunguza hata kumaliza kabisa vifo vya uzazi na watoto kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo(Ukumbi wa Nyerere), kitakachohusisha Halmashauri zote saba(7) za Longido.Meru,Arusha vijijini, Jiji la Arusha, Karatu,Monduli na Ngorongoro za mkoa wa Arusha na kinatarijiwa kufanyika kwa muda wa siku tatu..
Mhe. Mwaisumbe amesema kuwa inasikitisha kuona Mkoa kama Arusha kuwa miongoni mwa mikoa yenye tatizo hilo hapa nchini ukizingatia ni mkoa wenye watu wengi “Mkoa wa Arusha inasikitisha kuona unaongoza katika takwimu za vifo vya akina mama na watoto sijuhi ni wingi wa watu ama ni nini ila tunahitaji hatua za haraka” Mhe. Mwaisumbe.
Hata hivyo amefafanua serikali imekwisha liona hili na imekwishaanza utatuzi wa kujenga vituo vya Afya kuboresha hospitali za kawaida pamoja na za rufaa katika maeneo mbalimbali ya la Arusha ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kumaliza kabisa tatizo hili.
Awali akitoa mwongozo wa yatakayojadiliwa mbele ya mkuu wa Wilaya na wadau Daktari mkuu wa Wilaya longido Dk. Justice Munisi amebainisha kuwa takribani wakina mama 810 wana kufa kwa siku duniani na 90% ni kutoka katika jangwa la Sahara.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM