Vikundi viwili kutoka katika kata za Mundarara na Engarenaibor vimepatiwa mafunzo ya jinsi ya kunenepesha na kuhifadhi malisho na timu ya wataalamu kutoka idara ya mifugo Halmashauri ya longido
Vikundi hivyo ni DUPOTO kutoka kata ya Mundarara na ERETO kutoka kata ya Engarenaibor.
Akiongea wakati wa mafunzo hayo mkuu wa idara ya mifugo ndg.Nestory Dagharo amesema lengo kubwa la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wanavikundi hao jinsi ya kunenepesha na kuhifadhi malisho ya wanyama ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.Mradi huo umefadhiliwa na shirika la maendeleo (UNDP).
Nae mmoja wa wana vikundi hao amesema wanaishukuru sana serikali yao kwa kuwatafutia wafadhili hao kwani kwa sasa wana uhakika mifugo yao haitakufa na watakuwa na uhakika wa malisho lakini pia wamejifunza jinsi ya kunenepa mifugo na kuhifadhi malisho kwa ajili ya mifugo hiyo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM