Na Johnson Ismail
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. ICTO
Kikao cha kujadili fursa mbalimbali za kuinua na kutumia raslimali zilizopo kwa maendeleo ya wananchi wa Wilaya ya Longido kutoka kwa wadau hao,kikao hicho kimefanyika mapema hii leo katika ukumbi wa Mwalim J.K.Nyerere.
Kikao hicho kilicho endeshwa na Mkurugenzi Mtendaji Wakili Jumaa Mhina kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazo wakabili wananchi wa Wilaya ya Longido yenye Tarafa 4, Kata18, Vijiji49 na Vitongoji 176 Inayo kadiriwa kuwa na Wakazi142,597ya(sensa2017).
Mkurugenzi Mtendaji Wakili Jumaa Mhina alizungumzia frusa za uwekezaji zilizopo katika Wilaya kuwa ni Eneo lakupaki magari makubwa nje ya mji wa Namanga lenye huduma za chakula na malazi,Viwanda vya kusindika nyama&machinjio yakisasa, Viwanda vya kusindika maziwa na bidha zake,Agriculture produce border market,Petrol stations,Garage kwa ajili ya service za magari.
Pia Mkurugenzi Wakili Mhina alitoa frusa katika utoaji wa huduma za jamii ambazo ni ujenzi wa hospitali ya wilaya,Ujenzi wa miundo mbinu ya elimu ya sekondari Madarasa 20 kwa shule 10,nyumba 2 za Waalimu(6 in1),Mabweni 10 kati ya shule5 za sekondari.
Mkurugenzi Wakili Mhina alielezea changamoto mbalimbali za sekita ya Mifugo,Maendeleo ya jamii,Afya,Kilimo,Maji,Misitu,Biashara,Wanyama pori,Utawala bora,Ushirika na katika idara ya Elimu ya msingi.
Kikao kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Wilaya,Wadau walio shiriki ni Maasai primary,Driling water,Trians Tanzania,Muhesi Safari,Sido,L.D.P,UCRT-maisha bora,Heifer international,Madihani,ShirikaLOOCIP,Ujenzi,Chakula cha mifugo,PCI,Childreach(Tz),Pastoral womens council,Kilombero north safaris,Maisha bora,Afya,Anapa,Convois of AOPE,Fees.
Wadau hao walitoa mapendekezo yakuunda umoja wa wahisani wote wa ndani na nje ya Wilaya pia kutafuta watu wote walio soma katika wilaya ya Longido na kuwa kitu kimoja, kutumia rasili mali zinazo zunguka wilaya kuzibadili kuwa fedha,mawasiliano kuunda groap moja ili kujadili mambo ya maendeleo.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM