Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO) kwa kushirikiana na REPOA leo tarehe 12/04/2021 wamewapatia mafunzo ya uchakataji wa ngozi ya mifugo kwa wafugaji wadogo wadogo wa wilaya ya Longido.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank Mwaisumbe amesema wafugaji hawana budi kuhifadhi vizuri mazao yote yatokanayo na mifugo ikiwepo Ngozi, Pembe n.k na amewataka wafugaji kuuza mifugo yao ndani ya nchi ili tusipoteze malighafi zitokanazo na mifugo hiyo lakini pia kuongeza ajira kwa vijana.
Mkurugenzi wa REPOA aliwaambia wafugaji kwamba ubora wa ngozi na bidhaa zake unaanza tangu mfugaji anapoanza ufugaji na kuwachanja na kuwakinga na magonjwa yanayoharibu ngozi kama Minyoo pia jinsi wanavyoweka chapa kwenye mifugo lakini pia amewaeleza maeneo mazuri kwa ajili ya chapa kama miguu,nundu,sikio na paji la uso. Vilevile malisho bora ni muhimu maana mnyama anapokuwa na malisho duni hufanya ngozi yake kukosa thamani.
Wafugaji hao wamefurahia mafunzo hayo na kutaja changamoto yao kubwa ni maeneo ya malisho.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM