Ujenzi wa Mradi wa Kituo cha Afya Eworendeke unaendelea vizuri uko kwenye hatua ya upauaji bati majengo sita yameshapauliwa.
Majengo hayo ya Maabara,jengo la OPD, jengo la upasuaji ,Mochwari, jengo la kina mama na watoto,na nyumba ya mtumishi yanajengwa kwa kutumia Force Account inayoruhusu kutumia Local Fundi kwa usimamizi wa Kamati ya Ujenzi ya Kata ya Eworendeke chini ya uangalizi wa Wataalamu Washauri wa idara ya Ujenzi na Kitengo cha Manunuzi Halmashauri ya Longido.
Matumizi ya Force Account yanapunguza gharama za ujenzi kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na gharama kubwa za kutumia Wakandarasi wakubwa.
Njia hii pia inawezesha jamii inayozunguka kwenye eneo la mradi kupata kazi za kujiongezea kipato kwa kuwa fundi mjenzi ni lazima awe mkazi wa wilaya husika pamoja na kushirikisha jamii katika usimamizi wakati wote wa utekelezaji wa mradi.
Ushiriki wa Kamati ya Ujenzi ambayo inatokana na wananchi wakazi wa eneo husika inaongeza uwazi na jamii kutambua umuhimu wa mradi pamoja na kujimilikisha mradi kwa kuona kuwa mradi huo ni wao.
Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya cha eworendeke unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 700.
Aidha lengo la ujenzi vituo hivyo vya Afya ni kutoa huduma za haraka na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM