Na. Saumu Kweka
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. AgDICTO
Wananchi wa Kata zote za Wilaya ya Longido wameaswa kuweka akiba ya chakula kwa ajili ya matumizi ya baadaye kwa kipindi ambacho kutakuwa na upungufu wa chakula.
Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Bw. Edward Kasiga kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido amewataka Wananchi kuhifadhi chakula kulingana na idadi ya familia yake,kwa uwiano wa gunia 3 kwa mwaka kwa Mwananchi mmoja.Hivyo kila Kaya kuhifadhi kulingana na mahitaji yao.
Aidha Bw. Kasiga amewashauri Wananchi kutumia njia rahisi ya kutumia mifuko maalumu ya kuhifadhia mazao bila kuweka dawa kwa mwaka mzima bila kuharibika,ikiwa mazao hayo yamekaushwa vizuri na hayana unyevu unyevu.
Pia aliwashauri kujenga nyumba rahisi ambazo hazivuji katika kipindi cha mvua na kuweka kichanja ndani yake sehemu ambayo itatumika kuhifadhi mazao yao.
Katika msimu/kipindi hiki Wananchi wakiwa wanaendelea au wamekwisha kuvuna maeneo yao ya kilimo wanahimizwa kutumia mazao waliyopata kwa uangalifu ili kuepukana na baa la njaa,na pia wafugaji wanashauriwa kuuza baadhi ya mifugo na kujinunulia chakula na kukihifadhi kwa ajili ya matumizi ya kipindi ambacho kuna uhaba wa chakula
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM