Leo tarehe 25-03-2021 idara ya maendeleo ya jamii iliyochini ya Bi Grace Mghase imeendesha mafunzo kwa watendaji wa kata,walimu wa vikundi na maafisa mbalimbali ngazi ya wilaya kuhusu kutoa mwongozo wa usajili wa vikundi na jinsi ya kuandaa katiba ya vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha.
Kaimu mkurugenzi ndugu Joseph Logolie alifungua mafunzo hayo kwa kuwapongeza kuhudhuria kwa wakati na kuwataka wajumbe wote kushiriki mafunzo hayo kwa kusikiliza mada zote zinazotolewa na wawezeshaji ili kuhakikisha zoezi linakamilika kwa wakati.
Wawezeshaji kwenye mafuzo hayo ndugu Evans,Betty na Abunuas walitoa taratibu na kanuni mpya ya usajili wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha ambao kwa sasa usajili wa vikundi vyote vya kifedha utafanyika kwa njia ya mfumo wa kieleckroniki unaoitwa CMG Online Registration System unaopatikana kupitia link ifuatayo https://Cmg.bot.go.tz/cmg-portal.
Kwenye mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali kama Pastorial Women Council (PWC) inayojihusisha na kuwawezesha na kuwatambua wanawake waliokwenye jamii za kifugaji kuwainua na kuwakomboa kiuchumi kupitia miradi mbalimbali. Pia benki ya NMB nao walikuwepo kutoa mada fupi juu ya taratibu na masharti ya ufunguaji wa akaunti bila ya usumbufu.
Mwisho kabisa mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Bi.Grace Mghase alifunga mafunzo hayo kwa kutoa mikakati na taratibu rahisi za kuhakikisha usajili unafanyika kwa wakati kwa kuwataka kwanza watendaji wanahakikisha wanawahimiza viongozi wote wa vikundi wanaandaa viambata vyote vinavyohitajika ili usajili ukamilike pia kuwataka watendaji na walimu wa vikundi kuhakikisha elimu hii waliyoipata wanaipeleka kwa wanachama wote kwenye vikundi vyao.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM