Watendaji 18 wa Kata za Halmashauri ya, Wilaya ya Longido Leo tarehe 18/11/2022 wasaini mkataba wa Lishe ikiwa ni juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan za kupinga na kuzuia utapiamlo kwenye jamii ikizingatiwa lishe ni msingi wa afya ya binadamu, Maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Akifungua kikao hicho cha utiaji Saini wa Mikataba ya Lishe
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Afisa Tawala Wilaya ya Longido Ndugu Boniface Lugola Ameiasa jamii kuzingatia lishe bora kwa watoto ili kuimarisha afya ya mtoto mmoja mmoja ili kuondokana na magonjwa kwa watoto hususani utapiamlo ambao umekuwa tishio kwa watoto wengi
Pia amewataka Watendaji wa kata kuifanya agenda ya Lishe iwe ya kudumu kwenye Mikutano yao Kwa kushirikiana na wataalamu wa Lishe kwa kutoa Elimu juu ya Lishe bora kwa jamii
Nae mkuu wa idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na lishe Dr Selemani Mtenjela ameiomba jamii hasa wakina mama kuzingatia unyonyeshaji wa mtoto kwa muda wa miezi sita kwani ndio msingi mkubwa wa lishe na Afya ya mtoto sambamba na hilo ameomba pia mtoto apewe chakula bora chenye vitamin zote ili kumsaidia katika ukuaji wake ili kuondokana na Maradhi yanayohusiana na ukosefu wa chakula bora.
Serikali imejitahidi sana katika kutoa misaada mbali mbali kwa jamii hususani chakula ili kusaidia kuondokana na baa la njaa kwa jamii ivyo kuwataka wajumbe kuhamasisha jamii kuzingatia mlo ulio kamili alisema ndugu Edward Mboya kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Longido.
Zoezi hilo la utiaji saini mikataba ya lishe limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri na kushuhudiwa na wakuu wa Idara na Vitengo na Kamati ya uendeshaji huduma za afya ngazi ya Wilaya.
#Kazi iiendelee#
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM