Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango , halmashauri ya Longido imefanya ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne cha April-June, kwa mwaka wa fedha 2017/18.
Ziara hiyo ni ya kisheria yenye lengo la kukagua na kujionea utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo katika maeneo ya vijiji na kata ndani ya halmashauri.
Jumla ya miradi mbalimbali 18 kwenye sekta ya Elimu, Afya ,Maji na Mifugo imetembelewa ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi na maabara za science shule ya sekondari kitumbeine,ujenzi wa nyumba ya watumishi na madarasa matatu shule ya msingi kitumbeine,ujenzi wa kituo cha afya kitumbeine, ujenzi wa maabara za science na madarasa mawili shule ya sekondari Engarenaibor ,Ghala la kuhifadhia chakula, Maabara ya mifugo na ujenzi wa Kituo cha afya Engarenaibor na ujenzi wa shule ya sekondari Matale, ujenzi wa wodi ya wazazi kituo cha afya ngereyani na bweni la wanafunzi shule ya msingi ngereyani, mradi wa maji wa mto simba, ujenzi wa nyumba ya mtumishi shule ya msingi elerai,ujenzi wa mabweni mawili shule ya sekondari Enduimet, ujenzi wa ghala la mazao sinya na bweni na nyumba ya watumishi shule ya msingi sinya Ujenzi wa jengo la XRAY kituo cha afya Longido,jengo la jenereta na ukaguzi wa jenereta kituo cha afya Longido, ujenzi wa kituo cha afya Eworendeke, ukarabati wa Tanki la maji Namanga, ujenzi wa kiwanda cha nyama Eworendeke,mnada wa mifugo wa Eworendeke na tanki la maji Orbomba.
Hata hivyo wajumbe wa kamati hiyo ya fedha wametoa ushauri na maagizo mbalimbali lakini pia wameendele kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo huku wakiwapongeza wataalam na wananchi kwa kujitoa kwa hali na mali wakati wa utekelezaji wa miradi katika maeneo yao.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM