MRADI WA MAJI MTO SIMBA-Longido
Serikali imedhamiria kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama Wilayani Longido kwa kuanzisha Mradi mkubwa wa maji kutoka katika chanzo cha Mlima Kilimanjaro hadi kufika katika makazi ya wananchi.
Maji hayo yanatoka katika chanzo cha maji cha mto Simba kipo Wilayani Siha,Mkoani Kilimanjaro,kilomita 64 hadi Longido.
utekelezaji wa Mradi huu mkubwa umegawanyika katika miradi midogo midogo minne ,ambayo ni kutoka chanzo kikuu hadi Longido mjini,kinachogharimu jumla ya shilingi billioni10,890,000,000,Utekelezaji wa pili wa mradi ni ukarabati wa matanki mawili makubwa yaliyopo Longido mjini na kupeleka maji katika kijiji cha Engikareti kitakachogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,539,752,938.Utekelezaji wa tatu ni Ujenzi wa Tanki kubwa Longido mjini lenye ujazo wa lita laki 450 utakaogharimu kiasi cha shilingi 276,355,771.20 na mradi wa mwisho ni kusambaza mabomba kilomita 44.9 Longido mjini utakaogharimu shilingi bilioni 2,087,830,435.00.
Changamoto zinazoukakabili mradi huo ni upimaji uliofanyika mwaka 2014 na utekelezaji wa mradi kuja kufanyika mwaka 2017, changamoto nyingine ni Miundombinu ikiwa ni baadhi ya mabomba kupita katika eneo la hifadhi ya Misitu ya Serikali na kulazimika kutafuta kibali kutoka mamlaka ya uhifadhi wa misitu.
Vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni pamoja na Engikareti,Oltepes,Orbomba,Longido na Ranchi vyenye jumla ya idadi ya Wakazi elfu 29.
Mradi huu unatarajia kukamilika Disemba mwaka huu.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM