RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MRADI WA MAJI SAFI LONGIDO
Posted on: October 18th, 2021
Mhe. Rais Samia leo tarehe 18-10-2021 amehutubia wananchi wa wilaya ya Longido katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Stendi Mpya ya Longido mkoani Arusha mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama uliogharimu shilingi bilioni 15.8 na kufungua kiwanda cha nyama cha Elia Food Overseas Ltd chenye gharama ya Tshs Bilion 17.