Leo tarehe 16/10/2019 Halmashauri ya wilaya ya Longido imeendeleza desturi yake ya kutoa Mikopo kwa makundi mbalimbali ya walemavu, wanawake na vijana ikiwa ni agizo la serikali ikitaka kila Halmashauri kutenga asilimia 10% ya mapato ya ndani kwa ajili ya vikundi hivyo.
Jumla ya vikundi 17 vilivyomo ndani ya wilaya ya Longido vimenufaika na mkopo huo wa takribani milioni hamsini (50,000,000/=) uliotolewa na halmashauri.
Afisa maendeleo ya jamii wilaya Bi Grace Mghase alisema wilaya ya Longido ina takribani vikundi 541 vilivyosajiliwa ikiwemo 11 watu wenye ulemavu, 105 vijana na 425 wanawake vyote hivi vinajishughulisha na uzalishaji mali na vyote vinaratibiwa na kusimamiwa na idara ya maendeleo ya jamii. Pia alisema kuwa halmashauri inaendelea kutekeleza agizo la serikali la asilimia 10 ya mapato ya ndani kurudishw kwa jamii kwa kuwapatia mkopo usio na riba. Mwisho alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/2019 halmashauri ilitoa mkopo wa kiasi cha shilingi 132,630,000 kwa vikundi mbalimbali na mwaka huu wa fedha 2019/2020 wamepanga kutoa kiasi cha shilingi 150,000,000 ya pato la ndani.
vikundi vilivyonufaika na mkopo huo ni pamoja na Msanja – Namanga, Naserian Olokii - Ngereyani, Kipok Tengai B-Merugoi, Amani -Kamwanga, Namunyak -Mundarara, Juhudi -Longido, Kiserian -Oltepes, Nashipai - Lubwa, Tumaini -Kiserian, Ilanywaak – Ilerai, Nasyeku -Orkrjuloong, Dupoto – Owerendeke, Namanga Vijana Unity -Namanga, Memusi -Lumbwa, Kikundi cha Esupat Kitendeni -Kitendeni, Pamoja walemavu -Kitumbeine, na Kikundi cha walemavu Engusero -Engusero
Akikabidhi cheki ya kiasi cha shilingi milioni hamsini 50,000,000 taslimu mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh. Frank James Mwaisumbe, amesema Vikundi 17 mliopatiwa mkopo huo tayari fedha zenu zimeingizwa kwenye akaunti na Nawasihi mkatumie kwa jinsi mlivyo ainisha kwenye shughuli zenu bila kuathiri malengo ya vikundi vyenu na kurudisha fedha hizo kwa wakati ili na vikundi vingine viendelee kunufaika. Pia aliwaagiza watendaji wa mikopo kuhakikisha vikundi ambavyo vimeshapatiwa mkopo wasijirudie mpaka vikundi vingine nao wapate kwanza.
Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Ndg.Nestrory Dagharo ,amesema Vikundi vimepata mkopo wa jumla ya shilingi millioni 50 kwa ajili ya vikundi mbalimbali vya halmashauri ya wilaya yetu ,Nawasihi mkatumie kwa jinsi mlivyo ainisha kwenye shughuli zenu bila kuathiri malengo ya vikundi vyenu .
"Vile vile halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vingine mbalimbali katika halmashuri yetu hivyo basi nawasihi mkafanye kazi na mrudishe mkopo kwa wakati ili na vikundi vingine viendelee kunufaika"alisema kaimu mkurugenzi Nestory.
Nae Mbunge wa Longido Mh Steven Kiruswa amewaasa wanavikundi kutumia fursa hii vizuri wa ajili ya kuleta maendeleo na kubadilisha hali yao ya maisha. Pia Mbunge alishauri kuwa Vile vikundi ambavyo vitarudisha mkopo wake kwa wakati wapewe vipaumbele kwenye awamu nyingine ya mkopo ili kuwahamasisha vikundi vingine kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Pia vikundi hivyo kumi na saba 17 walipata nafasi ya kupewa semina ya ujasiriamali kutoka kwa mtaalam Mkurugenzi Isaak Mnyangi wa shirika la integrity Foundation Society. Wanavikundi wamefundisha vitu na mbinu mbalimbali za ujasiriamali kama vile kutengeneza batiki na kuwaasa wajasiriamali hao kuweza kujiajiri ili kuondokana na umasikini na utegemezi. Amehimiza kuwa vyanzo vya vya umasikini nchini ni kutokana na watu wengi kutokujishugulisha katika kazi mbalimbali pamoja na kutotumia fursa wanazo pata.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM