MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA LONGIDO. TAREHE 04.09.2019
Baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya Longido wakiwasilisha taarifa za utekelezaji wa kata kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2019. Hivyo leo tarehe 04.09.2019 kikao hicho kilicho ongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mhe. Sabore Molloimet katika ukumbi wa mikutano wa J.K. Nyerere Halmashauri ya wiliya Longido. Katika kikao hicho kila Diwani aliweza kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kata kwa kuelezea namna ya utekelezaji wa maazimio ya kikao kilicho pita mwezi Mei 2019, mafanikio, changamoto pamoja na mapato na matumizi katika kata zao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Longido Mhe. Sabore Molloimet amewaomba waheshimiwa madiwani kuandaa tarifa zao na kupeleka mahali husika kwa wakati, pia ameagiza watendaji kuwa na tabia ya kuwakumbusha waheshimiwa madiwani kusaini taarifa wanazoziandika, sambamba na hilo amewataka viongozi ( madiwani) kulinda usalama wa raia na mali zao kwani wananchi waliwachagua kwa kazi hizo.
Baada ya diwani wa Mundarara Mhe. Elias Mushao kuelezea jinsi kata yake ilivyo na uhaba wa vyombo vya uasafiri hasa kitengo cha afya ameeleza kuwa vijiji kumi na mbili (12) hutegemea zahanati moja , na kuulizia Pikipiki iliyo tolewa na mhe. Catherine Magige kwajili ya zahanati ya Mundarara, ndipo Mwenyekiti akatoa agizo kwa afisa ukaguzi kwamba pikipiki hiyo ipelekwe eneo husika maara baada ya kikao hicho. Diwani wa Kamwanga Mhe. Elias Mbao, ameomba Halmashauri ya wilaya kuweza kumpeleka mganga mkuu kata ya Kamwanga kwani kuna changamoto kubwa katika sekta ya Afya.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Longido wakili Jumaa Mhina, amelielezea baraza juu ya umeme wa vijijini ( REA) na kusema kuwa wilaya ya Longido pekee ndio haikupata mgao wa umeme vijijini kwa miaka iliyo pita ila kwasasa mgao huo wa umeme umefika wilayani Longido na tukiwa tumekusudia kila kata kuwa na umeme na kuwaomba waheshimiwa madiwani wakisaidiana na watendaji wa kata kutoa taarifa ya vijiji ambavyo hawajafikiwa na huduma ya umeme huu wa (REA). Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Longido, Mhe. Sabore Molloimet amesema kuwa ifikapo mwaka 2022 vijiji vyote wilayani Longido vitakuwa vinawaka umeme.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM