Mhe. Simon Oitesoi Laizer ameshinda kwa kishindo kikubwa kwa nafasi ya makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Longido, Mhe. Simon Oitesoi ambaye ni Diwani wa kata ya Gelai Lumbwa, ameshinda kwa kura nyigi za ndio zilizopigwa na waheshimiwa madiwani katika kikao cha mwisho wa mwaka kilicho fanyika leo tarehe 05.09.2019 katika ukumbi wa mikutano wa J.K. Nyerere ndani ya Halmashauri ya wilaya Longido. Akizungumza na Baraza la madiwani pamoja na wakuu wa idara za Halmashauri ya wilaya Longido alishukuru kwa nafasi walioweza kumpa ridhaa ya kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri kwa mwaka 2019 2020 zaidi ya yote aliomba ushirikiano mkubwa kwa viongozi wenzake ili kuwez kuwatumikia wana nchi wa Longido waliotuamini katika nafasi hizi. Pia alimshukuru sana Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mhe. Sabore Molloimet pamoja na Makamu mwenyekiti aliemaliza muda wake Mhe. Esupat Ngulupa kwa maendeleo waliofanya kwa kipindi chote cha uongozi. Katika kikao hicho cha uchaguzi kilicho simamiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya wakili Jumaa Mhina alisimamia uchaguzi wa kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri kamati hizo ni kamati ya Utawala fedha na mipango, Elimu afya na maji, kamati ya kuthibiti UKIMWI, Uchumi ujenzi na maingira pamoja na kamati ya maadili ya madiwani. Uchaguzi huo uliosimamiwa na wakili Jumaa Mhina uliofuata kanuni na sheria za Nchi na hata za Halmashauri ya wilaya kamati zote teule zilipewa nafasi ya kukaa na kumchagua mwenyekiti wake. Ambapo baada ya kamati hizo kuwapata wenyeviti waliounda kwapamoja kamati ya fedha Mwenykiti wa Halmashauri ya wilaya Mhe. Sabore Molloimet aliwashukuru viongozi wenzake kwa uwajibikaji na kupongeza Mhe. Simon Oitesoi kwa nafasi aliyo weza kupata kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Longido pia alisisitiza kwa waheshimiwa madiwani kuwa hakuna kamati iliyo bora kuliko nyingine kamati zote ni sawa na zote hufanya kazi ili kuendeleza wilaya yetu kwapamoja. Katibu tawala wa wilaya ya Longido Toba Nguvila alisema kuwa uchaguzi huu uliofanyika ni wa haki na demokrasia pia alimpongeza mhe. Makamu mwenyekiti Simon Oitesoi kwa kuweza kushinda nafasi hiyo, alimshukuru pia aliyekuwa makamu Mwenyekiti Esupat Ngulupa kwa kuonyesha uwezo mkubwa wa kiuongozi kwa muda mrefu amesema kuwa katka jamii za kifugaji mwanamke kuongoza kwa nafasi kubwa kama alivyo kuwa Ngulupa inaonyesha ukuwaji mkubwa wa kidemokrasia hivyo alisema kuwa ana imani pia na makamu mwenyekiti wa sasa Mhe. Simon Oitesoi kwani ana msimamo na ni mchapa kazi.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM